Qur’ani Ni Mawaidha, Tiba, Uongofu Na Rehema

| |times read : 606
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Qur’ani Ni Mawaidha, Tiba, Uongofu Na Rehema

 

       Hapa nitafupisha maneno aliyo yataja Sayyed Tabatabai katika tafsiri ya aya ya 138 katika surat Al-Imran[1]:

       Raghibu anasema katika kitabu chake cha Al-Mufradat: “Neno alwa’dh, maana yake ni kukemea kunako ambatana na kuhofisha”. Na Khalili anasema: “Neno alwa’dh, maana yake ni ukumbusho wa jambo la kheri kiasi cha moyo kulainika”. Ama “Poza yay ale yaliyomo vifuani” ni kinaya cha kwamba Qur’ani inaondosha sifa mbaya za kiroho ambazo humsababishia mwanadamu uovu, humharibia maisha yake ya furaha na kumzuilia kheri ya dunia na akhera. Ama ni kwanini Mwenyezi Mungu ametumia neno vifua? Jibu ni kwamba: kwa kuwa watu wanajua moyo upo kifuani na wanajua kuwa mwanadamu hufahamu na kudiriki mambo kwa moyo wake na kuyatia akilini, hupenda na hukasirika kwa moyo wake, kama ambavyo hutaka, huchukia, hutaraji na hutamani kwao, ndo maana wakakihesabu kifua kuwa ni sanduku la yaliyo moyoni miongoni mwa siri na sifa za nzuri na mbaya kiroho zilizo ndani ya mwanadamu.

       Ninasema kuwa: hadithi zinonyesha kuwa Qur’ani ni poza na shifaa ya baradhi ya mwili pia. Baadi ya hadithi zinaeleza kuwa, surat Al-Fatiha lau itasomwa kwa maiti mara sabini kisha akafufuka lingekuwa ni jambo la kushangaza.

       Rehema ni hisia ya moyo inayo patika kwa kuona madhara au mapungufu kwa mtu mwingine, zikamsukuma kutaka kumuondoshea madhara au upungufu ule. Lakini sifa hii inahusishwa na Mwenyezi Mungu aliye takasika, huwa na maana ya kuhurumia mojo kwa moja bila kuanza kuhisia, kwa sababu Mwenyezi Mungu ameepukana na hisia, na hivyo hutumika sifa ya huruma kwake ikimanisha utoaji wake na unemeshaji wake kwa viumbe vila ulazima kuwa hisia.

      Huu ni upande mmoja tu katika kuyafafanua majina matukufu ambayo hayawezi huhusishwa na Mwenyezi Mungu kama yanavyo nasibishwa kwa viumbe.

      Unapo zichukua sifa hizi nne za Qur’ani ambazo zimetajwa na Mwenyezi Mungu, namanisha sifa ya kuwa Qur’ani ni: mawaidha, pozo ya yale yaliyomo vifuani, uongofu na rehema, kisha ukazipima baadhi yake kwa baadhi, halafu ukazihusisha na Qur’ani, aya hiyo itatoa ubainifu unao kushanya athari zote nzuri na matendo yake masafi inayoyaweka katika nafsi za waumini tangu kuanzia inaposikika masikioni mwao hadi inapojikita ndani ya nyoyo zao.

       Kwa hakika Qur’ani jambo la kwanza kabisa ilifanyalo kwa waumini baada kughafilika, na kuzingirwa na sintofahamu kiasi cha uwepo wao kuzungukwa na giza la mashaka, na pale nyoyo zao zinapo patwa na maradhi yatokanayo na kila aina ya sifa mbaya au hali mbaya, Qur’ani huwawaidhi kwa mawaidha mazuri, huwazindua na kuwatabahisha waamke kutoka katika usingizi huo wa kughafilika, kama ambavyo huwakemea waachane na tabia mbovu na matendo mabaya, na hatimae kuwahimiza kuiendea kheri na furaha na dunia na akhera. Kisha huanza kuhizisafisha nyoyo zao na kila sifa mbaya, na itaendelea kuondoa maafa ya akili na maradhi ya nyoyo moja baada jingine mpaka zimelizike.

       Kisha Qur’ani huwaonyesha waumini hao mafunzo ya haki na maadili mazuri na matendo mema kwa upole na kuwainua daraja moja baada jingine na huwazogeza kwenye cheo baada ya kingine mpaka huwafikisha kwenye kituo cha walijikarisha kwa Mwenyezi Mungu, na hapo watafauli ufaulu wa watu wenye nia safi.

       Qur’ani haishii hapo, bali huwavisha vazi la rehema na huwakaribisha kwenye nyumba ya utukufu na huwakalisha kwenye masofa ya furaha na itawakutanisha na manabii, na masiddiki,na mashahidi na watu wema, na hao ndio marafiki wema. Kisha itawaingiza katika kundi la waja walio karibu na Mwenyezi Mungu katika pepo za juu kabisa.

       Hivyo, Qur’ani ni muwaidhi, na tatibu wa yale yaliyomo vifuani, yenye kuongoza kwenye njia iliyo nyooka na yenye kutoa rehema kwa idhini ya Mwenyezi Mungu aliye takasika. Bali tunaweza kusema kuwa inawaidhi, na kuponya yaliyomo vifuani, na inaongoza na kutoa rehema yenyewe na sio kwa amri ya yeyote, kwa sababu yenyewe ndio sababu kiunganisha kati ya Mwenyezi Mungu na viumbe wake. Hivyo, Qur’ani ni mawaidha, na poza ya yaliyomo vifuani, na uongofu na rehema kwa waumini.        



[1]. Al-Mizan: jz: 10, katika tafsir ya aya 70-75 za surat Yuunus. Aya iliyo ikusudiwa na mwandishi ni ya 57 isemayo: “Enyi watu! Yamekufikieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu, na poza ya ale yaliyomo vifuani, na uongozo na rehema kwa wenye kuamini”.