Qur’ani Ni Kauli Nzito

| |times read : 433
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Qur’ani Ni Kauli Nzito

        Uzito ambao unabebwa na kauli au neno. Na Qur’ani ni nzito kwenye nafsi, kwa sababu huyazuwia matakwa ya nafsi na haiiachi uhuru, bali huiadabisha, huijenga na kuongoza. Qur’ani ni nzito kenye akili kutokana na siri na mambo kina ambao huwa vigumu kwa akili za watu wenye kiburi kuyavumilia na kuyabeba. Vilevile Qur’ani ni nzito kwenye roho ya mwanadamu, kwani ndani yake kuna sheria nzito na malezi ya aina tofauti tofauti. Bwana mtu (s.a.w.w) ameliashiria hilo pia alipo sema: “Surat Al-Hud na Al-Waqi’ah zimenizeesha. Kwa sababu yake kuna: “Simama sawa sawa kama ulivyo amrishwa”. Bila shaka alikuwa anajua uzito wa jambo hili ndio akasema hayo.

       Na chanzo cha uzito wa Qur’ani ni kwakuwa inatokea kwa Mwenyezi Mungu mtukufu. Na hili linaweza kuthibitishwa na nukuu za wanahistoria juu ya hali ya bwana mtume (s.a.w.w) pindi akiteremshiwa wahai (ufunuo). Sehemu nyingine uzito wa Qur’ani umesifiwa namna hii:

[لَوْ أَنزَلْنَا هَذَا الْقُرْآنَ عَلَى جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّهِ وَتِلْكَ الأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ]

Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur'ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri[1].

       Qur’ani ni nzito pia kutokana na mabalaa na matatizo yanayo msibu aliye ibeba (mtume) na yeyote anaye fanya juhudi za kuisimamisha katika jamii. Mwenyezi Mungu amesema:

[المص، كِتَابٌ أُنزِلَ إِلَيْكَ فَلاَ يَكُن فِي صَدْرِكَ حَرَجٌ مِّنْهُ لِتُنذِرَ بِهِ وَذِكْرَى لِلْمُؤْمِنِينَ]

Alif Lam Mym 'Saad, Kitabu kilicho teremshwa kwako - basi isiwe dhiki kifuani kwako kwa ajili yake, upate kuonya kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa waumini”[2]. Na ndio sababu ya bwana mtume (s.a.w.w) kuamrishwa kusimama usiku kwa ajili sala na ili kuwa karibu na Mwenyezi Mungu na kujenga mahusiano ya karibu kabisa na Mola mlezi wake mtukufu, kwa lengo kufanya maandalizi ya kuipokea kauli hiyo nzito na majukumu makubwa. Na Mwenyezi Mungu alimuahidi kuyapata matunda hayo kwa kusema:

[وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَى أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُوداً]

Na amka usiku kwa ibada; ni ziada ya sunna khasa kwako wewe. Huenda Mola wako mlezi akakunyanyua cheo kinacho sifika”[3].

 



[1]. Surat Al-H’ashri: 21.

[2]. Surat Al-A’araaf: 2.

[3]. Surat Al-Israa: 79.