Mwangalizi (Qayyim)

| |times read : 603
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Mwangalizi (Qayyim)

       Sifa hii inatokana na neno: “alqaymumah” lenye maana ya uangalizi. Hivyo, Qur’ani ni kitabu kinacho wasimamia waja wa Mwenyezi Mungu, ili kuwaongoza na kuwaonyesha masilahi na heri yao, ikiwa ni pamoja na kuwandaliwa kila aina ya furaha na mafaniko ya dunia na akhera, ni hii ni sawa afanyavyo msimamizi wa familia au jamii. Na njia inayotumiwa na Qur’ani katika usimamizi, ni msimamizi wa njia nyinginezo, sawasawa katika uuga wa itikadi au sheria. Ndio njia inayo ongoza njia zilizo salia, na hizo njia nyengine zinafuata njia ya Qur’ani. Kwa ajili hiyo, ikiwa mwanadamu atataka kheri na furaha hana namna zaidi ya kuuweka usimamizi wa Qur’ani maishani mwake, na si kama walivyo fanya leo hii kuipa mgongo na kuiacha njia Qur’ani, na badala yake wakazifanya akili za kibinadamu ambazo ni pungufu kuwa ndio hakimu wa maisha yao, akili ambayo mara nyingi hunyenyekea mbele matakwa ya nafsi na masilahi yakupita. Na ndio maana Mwwenyezi Mungu akaisifu Qur’ani kwamba, ndani yake hakuna upogo wala mafungufu, hakuna tatizo wala kasoro, akasema:

[وَلَمْ يَجْعَل لَّهُ عِوَجَا]

“... wala hakukifanya kina upogo (kombo)”[1]. Kwani miongoni mwa masharti ya anayetaka kumsimamia mwanadamu na kukamilisha mapungufu yake, yeye mwenye awe ni mkamilifu, kwani kama wasemavyo kuwa: “Asiye na kitu hawezi kutoa kitu”. Ni lazima msimamizi wa watu aisiwe na mapungu wala kasoro. Na sifa hii haipatikani isipokuwa kwenye Qur’ani na mwenza wake ambae ni kizito kidogo, yaani Ahlul-bayt (a.s). Na visivyo kuwa hivi viwili, havina haki ya kuongoza jamii na kuisimamia. Na haidithi zenye maana hii ni nyingi sana na zote zinatanguliza Qur’ani na Ahlul-Bayt (a.s).

 

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فإن لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً]

         “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa hakika atapata maisha yenye dhiki”[2], yaani maisha aliyo bana. Na hii ni sifa ya kila atakaye puuza ukumbusho na mawaidha ya Mwenyezi Mungu, kiasi kwamba akakata mahusiano yake na Mwenyezi Mungu na kishi mbali na Qur’ani tukufu, kwa hakika mtu huyo atakuwa na dhidi, mahangaiko na machukungu maishani mwake, kwakuwa atakuwa amejiondoa katika rehema za Mwenyezi Mungu zilizo enea kila mahali na atakuwa ni muhanga wa matamanio na tamaa ambavyo havina ukomo. Hivyo, ataishi akiwa na khofu ya mauti na hatimaye kukhasirika dunia ambayo ndio ilikuwa lengo lake na akhera hatakuwa na fungu. Ataishi akipupia kile alicho nacho akihofia kutoweka, ataishi kwa taabu kwakuwa hafuati isipokuwa sarabi (mazigazi), hapati chochote adganiacho mna faraha yake isipokuwa humbainikia kuwa alikosea na hivyo kufanya juhudi kutafuta kingine. Kwa mfano: atadhania kuwa furaha ataipata katika mali, atahangaika kukusanya mali hizo mpaka zitafikia mamilioni, lakini haipati ile furaha, atadhani labda furaha ataipata kwenye manyumba ya fahari, ataanza kujenga manyumba ambayo jicho halijawahi kuyaona, lakini pia huko  nako hataipa furaha yake, wakati huo atadhani furaha imo kwa wanawake, anastarehe nao kadiri awezavyo, mara anajikuta kafika kwenye njia iliyo fungwa, na hapo ndio kauli yake Mwenyezi Mungu itamhusu: “Alipo uona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola mlezi wangu.”, na mwezi hapa ni kinaya ya mali, atadhania mali ndiyo Mola mlezi wake mwenye kumletea furaha, Mwenyezi Mungu anasema: “Na ilipo tua” na akafeli kuipata ile furaha, “akasema: Siwapendi wanao tua”, “Na alipo liona jua limechomoza”, hapa jua ni kinaya ya mambo mengine ya dunia, “akasema: Huyu ndiye Mola mlezi wangu. Huyu mkubwa kiliko wote”,  huyu ndiye atakaye nipa furaha na utulivu wa moyo kwa kuwa ni mkubwa zaidi ya wote.

       Na sehemu muhimu na yenye taathira kubwa ni “Ilipo tua” na Mola huyu mlezi mpya akafeli kuleta furaha “akasema: Siwapendi wanao tua”, mamola wapungu wasio miliki heri hata ya nafsi zao achilia mbali kumiliki madhara au manufaa ya wasio kuwa wao.  Ifikia hapa, ikiwa mtu atakuwa mwenye moyo safi na nia njema katika kutafuta ukweli, basi hakika mtu huyo ataipata hidaya na uongofu, na atasema maneno ya waumini kwamba:

[قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ، إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ حَنِيفًا وَمَا أَنَاْ مِنَ الْمُشْرِكِينَ]

Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo fanyia ushirikina. Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliye ziumba mbingu na ardhi, wala mimi si miongoni mwa washirikina”[3]. Lakini kama hatakuwa na nia jema na ikhlasi, atandikiwa uovu na wakati huo majibu yake yatakuwa:

 

[وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَعْمَالُهُمْ كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاء حَتَّى إذا جَاءهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئًا وَوَجَدَ اللَّهَ عِندَهُ فَوَفَّاهُ حِسَابَهُ واللهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ]

“Na walio kufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote. Na atamkuta Mwenyezi Mungu hapo naye amlipe hisabu yake sawa sawa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.[4]

      Na hivyo atabakia katika uovu akiwa na mikosi na dhiki hali ya kuwa yumo baina nyundo ya kifo ambayo inaweza kummaliza muda wowote, na adhabu ya kupana tamaa: “Na hakika utawaona ni wenye kuwashinda watu kuliko wote kwa pupa ya kuishi”[5]. Wewe mwenyewe unashuhudia kuwa matukio mengi ya kujinyonga yanatokea katika nchi zilizo endelea kiuchumi na ambazo watu wake huishi kwa kujaza matumbo.

 

[قَدْ جَاءكُم مِّنَ اللّهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ، يَهْدِي بِهِ اللّهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلاَمِ وَيُخْرِجُهُم مِّنِ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ]

       “Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na kitabu kinacho bainisha. Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama, na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake, na huwaongoa kwenye njia iliyo nyooka.[6]” Basi Qur’ani ni nuru iumurikayo moyo wa muumini kwanza kasha kusafisha na uchafu wa maasi na madhambi, kasha kuuacha ukurasa wake uking’aa ili tayari kuingia haki ambayo ndio nuru ya umma na jamii itakayo iongoza kwenye mfumo utakayo uletea furaha na saada.

       Miongoni mwa ibara za Qur’ani ninazo vutia, ni kwamba neno “nur” lenye maana ya nuru au mng’o, imelileta likiwa na sura ya umoja, wakati neno giza limekuja kwa sura ya wingi. Na sababu yake ni kuwa njia ya haki ni moja tu hata kama mifano yake ni mingi. Mwenyezi Mungu anasema:

[اهدِنَا الصِّرَاطَ المُستَقِيمَ]

Tuongoze njia iliyo nyooka[7], wakati magiza yako mengi kama walivyo wengi miungu wanao zuilia na kuziba njia ya Mwenyezi Mungu.

          Katika athari na baraka za Qur’ani ni kuwa humuogoza mwenye kufuata radhi za Mwenyezi Mungu kwenye njia za amani. Na amani ya kwanza anayo neemeka nayo ni amani ya nafsi, utulivyo wa moyo na utakaso wa akili:

[أَلاَ بِذِكْرِ اللّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ]

“Kwa hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mumgu ndio moyo hutua”[8]. Kisha inafuatia amani ndani ya familia iliyo simamia misingi ya Uislamu na mafuzo ya Qur’ani:

[وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَلِكَ لآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ]

“Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri”[9]. Na baadae ni amani baina ya wanajamii, pale yanapo tawala mafunzo na adabu za Kiislamu:

[فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَاناً]

 “Kisha kwa neema yake mkawa ndugu”[10],  

[مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاء عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاء بَيْنَهُمْ ]

“Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao”[11] na

[وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ]

“Bali wanapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji”[12].



[1]. Surat Al-Kahf: 1.

[2]. Surat Taha: 124.

[3]. Surat Al-An’am:76-77.

[4]. Surat An-Nur: 39.

[5]. Surat Al-Baqarah: 96.

[6]. Surat Al-Maidah: 15-16.

[7]. Surat Al-Fath: 6.

[8]. Surat Ar-Ra’d: 28.

[9]. Surat Ar-Rum: 21.

[10]: Surat Al-Imran: 103.

[11]. Surat Al-Fath: 29.

[12]. Surat Al-Hashr: 9.