Kitabu Kitukufu (Almajiid)

| |times read : 555
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Kitabu Kitukufu (Almajiid)

 

       Raghibu anasema katika kitabu chake cha Al-Mufradat: Neno: “Almajdu”: ni upana katika ukarimu na utukufu. Na asili ya neno hilo ni kauli ya warabu: “majadat al-ibilu”, pale ngamia anapokutwa kwenye malisho yenye nyasi nyingi na makubwa. Hivyo, Qur’ani imesifiwa kwa sifa hii ya “majiid” kwa sababu ya wingi wa mema ya dunia na akhera iliyo yabeba.  Na ni kwa sabubu hiyo hiyo Mwenyezi Mugu akaisifu kwa kusema:

[إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ]

“ Bila shaka hii ni Qur’ni tukufu”[1],  kwa sababu ya kheri zake zinazo patikana kwa wingi, na hili tumeliashiria wakati tukifafanua athari tele za sifa “mubaarak”.



[1]. Surat Al-Hadid: 77.