Kitabu Chenye Nguvu (Al-A’ziz)
Kitabu Chenye Nguvu (Al-A’ziz)
1. Kwa maana kwamba Qur’ani ni kitabu ambacho ni vigumu kufikia uhakika wake. Kwani kitabu ambacho uhakika wake umehifadhiwa kwenye lohi mahfudhi, na matamshi yake chombo tu cha kuziweka maana zake karibu na akili ya kibinadamu iliyo zoea mambo ya kimada, na isiyo weza kuufikia ule uhakika wenyewe kama ulivyo. Ndio, wanao weza kuufikia na kuufahamu uhakika huo, ni wale tu walio takasika na ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na akawasafisha barabara, ambao si wengine bali ni Ahlul-bayt (a.s). Bila shaka umemsikia Amirulmuunina Ali (a.s) akisema: Kwa hakika sisi hatumiliki elimu zaidi ya ufahamu wetu wa Qur’ani.
2. Nacho ni kitabu chenye nguvu kwa maana ya kwamba, ni nadra kupata mfano wake, kwani ni maneno ya asiye kuwa na mfano.
3. Ni kitabu chenye nguvu kwa maana kwamba, kaiwezekani kikapwa na jambo baya. Na hivyo maana yake itakuwa ni sawa na aya hii:
[إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ]
“Hakika sisi ndio tulio teremsha ukumbusho huu, na hakika sisi ndio tutakao uhifadhi”[1].
4. Qur’ani ni yenye nguvu kwa maana kwamba ni kitabu chenye kushinda, kwa sababu ni neno la Mwenyezi Mungu, na neno la Mwenyezi Mungu ndilo lipo juu. Hivyo, Qur’ani ni yenye kushinda na wala haishindwi, nafasi yake ni kuwaongoza na kuwatawala waja kwa kutoa mwelekeo wa mambo yao.
5. Ni kitabu chenye nguvu kwa maana kwamba ni chenye kutafutwa. Kwani imesemwa kuwa: Kila kilichopo huchokwa na kila kilicho potea hutafutwa. Na Qur’ani hii ni yenye kutafutwa na kila atakae kufika kwa Mwenyezi Mungu aliye tukuka.
[1]. Surat Al-Hijr: 9.