Kitabu Kilicho Barikiwa

| |times read : 510
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Kitabu Kilicho Barikiwa

Yaani Qur’ani ina baraka tele. Na hivyo ndivyo ulivyo ukweli, na baraka zake zinaweza kuelezewa katika pande kadhaa:

1.       Qur’ani ina baraka kwa upande wa chanzo chake na pahali iliko tokea. Kwa sababu aliye iteremsha ni Mwenyezi Mungu  aliye tukuka, mtenda wema kwa waja wake mtoa neena sozizo na ukomo wala hesabu.

2.       Ni yenye baraka  kwa ilipo teremkia. Imeteremkia kwenye moyo wa bwana mtume mwenye huruma, aliye tumwa kuwa rahma kwa walimwegu.

3.       Qur’ani imebarikiwa pia kwenye athari zake. Ndini yake mna hidaya, heri na furaha ya dunia na akhera. Ndani ya Qur’ani mna mfumo na nidhamu ya maisha ya nwanadamu, mna misingi na ulinzi wa maisha, mna amani na utulivu.

4.       Kadhalika Qur’ani imebarikiwa kwa upande wa hajimu na kiasi chake. Ni kitabu kimoja, lakini wasomi wote hunufaika nacho, kila mmoja huchukua ndani yake ikitakacho. Utamkuta msomi wa Usuli, mwanazuoni wa fikihi, msomi wa nahau, mwandishi, mwanafikra, mwanasiasa, msomi wa elimu ya jamii, msomi wa uchumi, daktari, mtunga sheria na mtawala, utawaona wote wakinufaika na Qur’ani, na kila mmoja akitoa hoja zake kwa kutumia aya za Qura’ni. Lakini pamoja na yote hayo, bado itabakia ni kitabu cha kudumu na chenye kutoa maafira. Na hii ni dalili ya kuwa iliteremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu maarifa yaliyomo ndani ya Qur’ani ni maarifa ambayo hayawezi kukusanya na vitabu kadhaa kama si vyote.

5.       Na mwisho kabisa, Qur’ani ina baraka kwa idadi waliyo ongoka kwayo, nyoyo zao zikanawirika kwayo na akili zao zikapata mwanga kwa baraka zake.