UFAFANUZI WA BAADHI YA SIFA ZA QUR’ANI
UFAFANUZI WA BAADHI YA SIFA ZA QUR’ANI
Lakini maelezo hayo kuhusu sifa za Qur’ani hayatoshezi. Hivyo, ninaona kuna udharura wa kuzitolea ufafanuzi wa ziada baadhi ya sifa hizo, ufafanuzi utakao kuwa na athari chanya kijamii na kimaadili, ama ufafanuzi wa sifa hizo katika nyanja zingine, tumeuacha kwa ajili ya vitabu vya tafsiri, kwenye aya zilizo zitaja. Na sifa hizi sizitaji kwa lengo la kuifahamu Qur’ani pekee, bali ninazifafanua ile huwafahamu Ahlul-bayt (a.s) pia, kwakuwa wao ndio wenza wa Qur’ani na kwa pamoja hutengeneza mihimili miwili isiyo farakana. Hivyo, ikiwa Qur’ani inasema kweli basi Ahlul-bayt nao wapo na haki na haki ipo nao. Qur’ani ni kitabu kisicho fikiwa na batil, na Ahlul-bayt nao ni maasumina walio hifadhiwa na kutenda dhambi. Na ikiwa Qur’ani ni msimamizi na mlinzi, Ahlul-bayt (a.s) nao pia wana usimamizi na mamlaka juu ya watu, kwani wao ndio viongozi wa na ni wabora zaidi kuliko nafsi zao. Na ufuatao ni ufafanuzi wa sifa hizo: