QUR’ANI YAJISIFU YENYEWE

| |times read : 562
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

QUR’ANI YAJISIFU YENYEWE

Ama jambo muhimu zaidi kuliko hayo ni kukusomeeni baadhi ya aya ambazo Qur’ani tukufu yajisifu kwazo ili tuitambue, kwani bila shaka yenyewe inajijua zaidi, na iweje isijijue wakati ni maneno ya mbora wa wasemaji? Kutokana na aya hizi hufahamika utukufu na hadhi ya Qur’ani hii, heshima na baraka zake:

[هَذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ]

1.       “Hii ni bayana kwa watu wote, na ni uwongofu, na mawaidha kwa wachamungu.[1]

[إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ ]

2.       “Hakika sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kwa alivyo kuonyesha Mwenyezi Mungu. Wala usiwe mtetezi wa mahaaini”[2].

[يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُوراً مُّبِينًا، فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُواْ بِاللّهِ وَاعْتَصَمُواْ بِهِ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِي رَحْمَةٍ مِّنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَاطاً مُّسْتَقِيماً]

3.       “Enyi watu! Umekufikieni ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na tumekuteremshieni nuru iliyo wazi. Ama wale walio muamini Mwenyezi Mungu, na wakashikamana naye, basi atawatia katika rehema yake na fadhila, na atawaongoa kwenye njia iliyo nyooka”[3].

[قَدْ جَاءكُم مِّنَ اللّهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ، يَهْدِي بِهِ اللّهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلاَمِ وَيُخْرِجُهُم مِّنِ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ]

4.       “Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anaye samehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Nuru na Kitabu kinacho bainisha. Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama, na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake, na huwaongoa kwenye njia iliyo nyooka.[4]

[وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُواْ التَّوْرَاةَ وَالإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيهِم مِّن رَّبِّهِمْ لأكَلُواْ مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم]

5.       Na lau wangeliishika Taurati na Injili na yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka wangelikula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno.[5]

[قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَسْتُمْ عَلَى شَيْءٍ حَتَّىَ تُقِيمُواْ التَّوْرَاةَ وَالإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ]

6.       “Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlio teremshiwa kutokana na Mola wenu Mlezi.[6]

[مَّا فَرَّطْنَا فِي الكِتَابِ مِن شَيْء]

7.       “Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote.[7]

[وَهَذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ َ]

8.       “Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa.[8]

[وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُواْ لَهُ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ]

9.       “Na isomwapo Qur’ani isikilizeni na mnyamae ili mpate kurehemewa.[9]

[يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاء لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ]

10.  “Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na posa kuponyesha yaliyomo vifuani, na uongofu, na rehema kwa waumini.[10]

[إِنَّ هَذَا الْقُرْآنَ يِهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ ]

11.  Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria waumini ambao wanatenda mema.[11]

[اللَّهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ ذَلِكَ هُدَى اللَّهِ يَهْدِي بِهِ مَنْ يَشَاء وَمَن يُضْلِلْ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ]

12.  “Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa.[12]

[وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ، لا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلا مِنْ خَلْفِهِ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ]

13.  Kwa hakika wanayo yakataa mawaidha haya yanapo wajia (wataangamia), na haya bila ya shaka ni Kitabu chenye nguvu na utukufu. Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa.[13]

[اللَّهُ الَّذِي أَنزَلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ وَالْمِيزَانَ]

14.  Mwenyezi Mungu ndiye aliye teremsha Kitabu kwa Haki, na Mizani.[14]

[وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ]

15.  Na hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yalioko kwetu, ni tukufu na yenye hikima.[15]

[وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ]

16.  Anaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shet'ani kuwa ndiye rafiki yake.[16]

[فَاسْتَمْسِكْ بِالَّذِي أُوحِيَ إِلَيْكَ إِنَّكَ عَلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ، وَإِنَّهُ لَذِكْرٌ لَّكَ وَلِقَوْمِكَ وَسَوْفَ تُسْأَلُونَ]

17.  “Basi wewe yashike yaliyo funuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye njia iliyonyooka. Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa.[17]

[هَذَا بَصَائِرُ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمِ يُوقِنُونَ]

18.  Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uwongofu, na rehema kwa watu wanao yakinisha.[18]

[أَفَلا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَى قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا]

19.  Je hawaizingatii hii Qur'ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?[19]

[ق وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ]

20.  Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu![20]

[وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ]

21.  “Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka?[21]

[إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ، فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ، لا يَمَسُّهُ إِلا الْمُطَهَّرُونَ]

22.  Hakika bila ya shaka hii ni Qur'ani tukufu, katika kitabu kilicho hifadhiwa, hapana akigusaye ila walio takaswa.[22]

[أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ]

23.  “Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu.[23]

[لَوْ أَنزَلْنَا هَذَا الْقُرْآنَ عَلَى جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعاً مُّتَصَدِّعاً مِّنْ خَشْيَةِ اللَّهِ وَتِلْكَ الأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ]

24.  “Lau tumeiteremsha hii Qur'ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeliuona ukinyenyekea, ukipasuka kwa hofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri.[24]

[وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلاً، إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلاً ثَقِيلاً

25.  “Na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo. Kwa hakika sisi tutakuteremshia kauli nzito.[25]

[بَلْ هُوَ قُرْآنٌ مَّجِيدٌ، فِي لَوْحٍ مَّحْفُوظٍ]

26.  “Bali hii ni Qur'ani tukufu . Katika ubao ulio hifadhiwa.[26]

[إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ، وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ]

27.  “Hakika hii ni kauli ya kupambanua, wala si mzaha.[27]

[الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنزَلَ عَلَى عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُ عِوَجَا، قَيِّماً لِّيُنذِرَ بَأْساً شَدِيداً مِن لَّدُنْهُ وَيُبَشِّرَ الْمُؤْمِنِينَ]

28.  Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amemteremshia mja wake kitabu, wala hakukifanya kina upogo. Kimenyooka sawa, ili kitoe onyo kali kutoka kwake, na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba watapata ujira mzuri.[28]

[وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَاناً لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدىً وَرَحْمَةً وَبُشْرَى لِلْمُسْلِمِينَ]

29.  “Na tumekuteremshia kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa waislamu.[29]

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فإن لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

30.  “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.[30]” 

       Hizi ni baadhi ya sifa na athari nzuri ambazo husifika nazo Qur’ani. Qur’ani ni kitabu kilicho barikiwa, kwenye ngvu na utukufu na kilicho tukuzwa. Qur’ani ni bayana, ni uongofu, ni mawaidha, ni rehema, ni tiba, ni ukumbusho, na ni nuru iliyo teremshwa kwa haki, ili kuhukumu baina ya watu na ili kiwaingize waumini katika rehema za Mwenyezi Mungu na fadhila zake, na ili kiwaongoze njia iliyo nyooka. Qur’ani ni kitabu kitukufu na chenye hekima, ni chenye kuwafumbua macho watu, ni kauli nzito, ni kipambanuzi cha haki na batili na wala sio mzaha. Hivyo, ukweli na uhakika wa Qur’ani umewekwa ndani ya matamshi yake, na matamshi ndio chombo kilicho hifadhi ukweli na uhakika huo. Matamshi ya Qur’ani ndio yanayo isogezea akili uhakika na zile maana za ndani, zile maana zilizo fichikana katika lohi iliyo mahfudhi (hifadhiwa), kiasi kwamba hakuna agusaye wala kufikia maana uhakika huo isipokuwa walio takaswa kutokana na madhambi na maasi, nyoyo zao zikasafika na kila aina ya uchafu kiasi cha kuweza kuakisi kikamilifu ukurasa wa lohi hiyo iliyo hifadhiwa. Ama wasio kuwa hao, hawana uwezo wa kuzifahamu isipokuwa kwa kile kiwango kidogo cha ukamilifu walio pewa. Anasema Mwenyezi Mungu:  

[أَنزَلَ مِنَ السَّمَاء مَاء فَسَالَتْ أَوْدِيَةٌ بِقَدَرِهَا]

“Ameteremsha maji kutoka mbingini kisha mabonde yakamiminika maji kwa kadiri na kiwango chake”[31].

       Watu wameamrishwa kuizingatia Qur’ani, kuisoma kwa mafungu, kushikamana nayo na kunyamanza pindi inaposmwa, na lau ingeli kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu basi wangeli kuta ndani yake hitilafu nyingi. Na lau wangeli ishika Qur’ani na waka ambatana nayo, hapana shaka wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao, na nyoyo zao zingeli nyenyekea na kulainika, na wangeli stahiki kheri nyingi kutoka kwa mola wao mlezi. Lakini ikiwa wataiacha wataishi katika maisha ya dhiki na watavamiwa na mashetani mpaka wawafanye kuwa marafiki wao, na nyoyo zao zitakuwa ngumu hata kufikia kuwa kama mawe au zaidi, kwani kuna mawe yanayo timbuka mito, na kuna mengine yanayo pasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya khofu ya Mwenyezi Mungu. Na nyoyo zilizo mbali na Qur’ani na utajo wa Mwenyezi Mungu aliye takasika ni ngumu zaidi kiasi kwamba ndani yake hayawezi kuingia hata tone la maarifa. Mwenyezi Mungu anasema:     

[وَتِلْكَ الأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ]

“ Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri”[32].



[1]. Surut Al-Imaran: 138.

[2]. Surat An-Nisaa: 105.

[3]. Surat An-Nisaa: 174-175.

[4]. Surat Al-Maidah: 15-16.

[5]. Surat Al-Maidah: 66.

[6]. Surat Al-Maidah: 68.

[7]. Surat Al-An’aam: 38.

[8]. Surat Al-An’aam: 92.

[9]. Surat Al-a’araaf: 204.

[10]. Surat Yuunus: 57.

[11]. Surat Al-Israa: 9.

[12]. Surat Az-Zumar: 23.

[13]. Surat Fussilat: 41-42.

[14]. Surat Ash-Shura: 17.

[15]. Surat Az-Zukhruf: 4.

[16]. Surat Az-Zukhruf: 36.

[17]. Surat Az-Zukhruf: 43-44.

[18]. Surat Al-Jaathiyah: 20.

[19]. Surat Muhammad: 24.

[20]. Surat Qaaf: 1.

[21]. Surat Al-Qamar: 40.

[22]. Surat Al-Waaqi’a: 77-79.

[23] Surat Al-Hadid: 16.

[24]. Surat Al-Hashri: 21.

[25]. Surat Al-Muzammil: 4-5.

[26]. Surat Al-Buruuj: 21-22.

[27]. Surat At-Taariq: 13-14.

[28]. Surat Al-Kahf: 1-2.

[29] Surat An-Nahli: 89.

[30]. Surat Taha: 124.

[31]. Surat Ar-Ra’d: 24.

[32]. Surat Al-Hijr: