TUNA HAJA YA KUREJESHA QURANI KWENYE MAISHA YETU

| |times read : 458
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

TUNA HAJA YA KUREJESHA QURANI KWENYE MAISHA YETU

       Leo hii tuna haja kubwa sana ya kurejesha ustawi ya Qur’ani kwenye maisha ya waislamu na kuitoa kwenye kutengwa, kiasi kwamba imefikia hatua uwepo wa Qur’ani umekuwa unaishia kwenye hitima zisomwazo kwa ajili ya marehemu na kuifanya kama kinga.

       Kumekuwa na msemo usemao kuwa :(Hakika mwisho wa umma huu hautaimarika isipokuwa kwa kile kilicho uimarisha mwanzo), na ni wazi kwamba mwanzo wa umma huu haukuimarika isipokuwa kwa Qur’ani, hivyo jamii ya kiislamu ikitaka kurudi kwenye msitari haina namna zaidi ya kurudi kwenye Qur’ani na kuiweka maishani mwake. Imepokelewa kutoka kwa Miqdad (Mwenyezi Mungu amridhie) kutoka kwa mtume wa Menyezi Mungu (s.a.w.w) aliposema:

 

(فإذا التبست عليكم الفتن كقطع الليل المظلم فعليكم بالقرآن فإنه شافع مشفع وماحل مصدق ومن جعله أمامه قاده إلى الجنة ومن جعله خلفه ساقه إلى النار وهو الدليل يدل على خير سبيل)

“Itakapo kupateni fitina mfano wa usiku wa giza, basi rudini kwenye Qur’ani (mshikamane nayo), kwani Qur’ani ni mwombezi ambaye uombezi wake utapokelewa, na yenye kutoa taarifa itakayo kubaliwa, mwenye kuiweka mbele yake inamongoza kwenye pepo, na mwenye kuiweka nyuma yake itampeleka motoni, Qur’ani muongozo unao ongoza kwenye njia bora zaidi”[1]. Na Imamu anasema katika moja ya khutba zake:

 

 (واعلموا أن هذا القرآن هو الناصح الذي لا يغش والهادي الذي لا يضل، والمحدث الذي لا يكذب، وما جالس هذا القرآن أحد إلا قام عنه بزيادة أو نقصان: زيادة في هدى ونقصان من عمى، واعلموا أنه ليس على أحد بعد القرآن من فاقة ولا لأحد قبل القرآن من غنى فاستشفعوه من أدوائكم واستعينوا به على لأواءكم فإن فيه شفاءً من أكبر الداء وهو الكفر والنفاق والغي والضلال فاسألوا الله عز وجل به وتوجهوا إليه بحبه ولا تسألوا به خلقه إنه ما توجه العباد إلى الله بمثله، واعلموا أنه شافع مشفع وماحل ومصدق وأنه من شفع له القرآن يوم القيامة  صدق عليه فإنه ينادي مناد يوم القيامة: (ألا إن كل حارث مبتلى في حرثه وعاقبة عمله غير حرثة القرآن)، فكونوا من حرثته وأتباعه واستدلوه على ربكم واستنصحوه على أنفسكم واتهموا عليه آراءكم واستغشّوا فيه أهواءكم).

 

“Na tambueni kwamba Qur’ani hii ni mnasihi asiye haini, na kiongozi asiye potosha, na msemaji asiye ongopa, na hakuna aliye kaa na Qur’ani (aliye soma Qur’ani) isipokuwa alipo simama (alipo maliza kuisoma) oungofu wake uliongezeka na upotovu wake ulipungua. Na tambueni kwamba, hakuna muhitaji baada ya kujifunza Qur’ani, na hakuna aliye tosheka kabla ya kujifunza Qur’ani. Basi, yatibuni maradhi yenu (ya dhahiri na yaliyo jificha, ya kiroho na kimwali) kwa Qur’ani, na katika matatizo yenu ombeni msaada kupitia kwayo, kwani ndani yake kuna tiba ya maradhi makubwa zaidi, ambayo ni ukafiri, unafiki na upotofu. Hivyo, muombeni Mwenyezi Mungu kwa Qur’ani na mjielekeze kwake kwa kuipenda, kwani waja hawamwelekei Mwenyezi Mungu   kwa chochote kile kama wamuelekeavyo kwa Qur’ani, na kamwe msiombe viumbe wake kwa Qur’ani. Tambueni kuwa Qur’ani ni mwombezi ambaye uombezi utakubaliwa na ni mtoa ripoti anaye sadikiwa, na mwenye kuombewa na Qurani siku ya Kiyama uombezi wake utakubaliwa, kwani siku hiyo mwenye kunadi atanadi kwa kusema:  “Tambueni kwamba kila mkulima atatihaniwa kwa kazi yake isipokuwa wakulima wa Qur’ani”, hivyo kuweni miongoni mwa wakulima wa Qur’ani na wafuasi wake na ifanyeni kuwa muongozo wa kukupelekeni kwa Mola wenu Mlezi, na muitake nasaha kwa ajili ya usalama wa nafsi zenu, na zituhumuni fikra zenu kwa Qur’ani na matashi yenu mbele yake yahesabuni kuwa ni hiyana”[2].



[1]. Al-Kafii: 2/299.

[2]. Nahjul balagh, sharhi ya Mohammad Abduhu: 1/347. Khutba: 177.