QUR’ANI NI NJIA IKUFIKISHAYO KWENYE KUMTAMBUA MWENYEZI MUNGU

| |times read : 501
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

QUR’ANI NI NJIA IKUFIKISHAYO KWENYE KUMTAMBUA MWENYEZI MUNGU

 

       Yeyote yule amtakae Mwenyezi Mungu, na akawa anahitaji kufika kwake, ni wajibu wake ashikamane na Qur’ani, kwani jambo la kwanza katika dini ni kumtambua yeye. Imepokelewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) kwamba: “Hakika Mwenyezi Mungu amejionyesha kwa viumbe wake kupitia maneno yake (Qur’ani), lakini hawamuoni”[1]. Na anayetaka kujenga na kutakasa nafsi kutokana na maradhi yake mbali mbali, ni wajibu wake pia ashikamane na Qur’ani. Hali kadhalika, mwenye kutaka ustawi wa jamii yake na kuisimamisha kwa misingi ya amani, furaha na utulivu, naye pia analazimika kuishikilia Qur’ani. Kwa sababu Qur’ani ndio njia ya uongofu na kiongozi wa kila heri na wema.

 

       Inastaajabisha kuona kwamba kifaa chako kinapo haribika unakichukua kwa aliye kiunda ili akirekebishe, kwa kuwa aliye kitengeza kitu ndio mwenye ujuzi nacho zaidi. Na unapo ugua unaenda kwa daktari bingwa ili akutibu. Lakini unapo taka kurekebisha nafsi ya binadamu iliyo sheheni mambo mengi yaliyo fichikana kwa mwenye nafsi hiyo, achilia mbali asiyekuwa mwenye nayo, au unapo hitaji kuweka nidhamu na mfumo utakao dhamini furaha ya mwanadamu na kumrekebisha, eti unaenda kutafuta hilo kwa mwanadamu huyo huyo mwenye mapungufu na asiye jiweza, badala ya kwenda kwa muumbaji wa mwandamu huyo na mjuzi wa nafsi ya alichokiumba ili akupe muongonzo!

       Uzoefu wa Qur’ani katika kujenga nafsi na jamii, ulithibitika kwa bwana mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w). Kwani kuna ulingano mdogo tu, baina ya jamii ya kabla ya Uislamu na ile ya baada ya Uislamu, na mabadiliko makubwa yaliyo patikana kutokea kwenye jamii ya watu waliokuwa nyuma kitamaduni, wakiwa wamesambaratika,  na maovu yakiwa yametapakaa baina yao, wakijifakharisha kwa matendo maovu na machafu, mpaka kufikia hatua ya kuwa ni jamii iliyo endelea, yenye tamaduni, maadili mema na nidhamu ambayo haikuwahi wala haitakuja tokea mfano wake kwa jamii iliyojitenga mbali na Mwenyezi Mungu, ndani ya muda mfupi, yote hayo hayakutokea isipokuwa kwa baraka ya kitabu hiki kitukufu, na msimamizi wake mbora wa viumbe.



[1] . A’waalil- Alaalii:4/116.