WASIA WA KUHIFADHI QUR’ANI

| |times read : 542
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

WASIA WA KUHIFADHI QUR’ANI

     Yasiwaghuri madai ya wasemao kwamba, wao ndio wenye kuijali zaidi Qur’ani kuliko sisi[1]. Ninasema: hifadhini Qur’ani kwani ina hadhi ya kuhifadhiwa na kufanyiwa kazi. Kuweni kama alivyo kuusieni Amiirul muunina Ali bin Abi Talib (a.s) kabla ya kufariki kwake kishahidi:

 (الله الله بالقرآن لا يسبقكم إلى العمل به غيركم)

“Ninamuapa Mwenyezi Mungu ninamuapa Mwenyezi Mungu kuhusiana na Qur’ani. Asiyekuwa nyinyi asikutangulieni kuifanyia kazi”[2], na kama ilivyo katika usia wa mtume (s.a.w.w) kwa  Imamu Ali (a.s) akimuusia kuzifanyia kazi hadithi arobaini, alisema:

(وأن تكثر من قراءة القرآن وتعمل بما فيه).

“Na ukithirishe (uzidishe) kuisoma Qur’ani na kuyafanyia kazi yaliyomo ndani yake”[3].



[1]. Ninasisitiza sana juu ya nukta hii, kwa kuwa watu wengi wakaiwaida na wasiokuwa na ujuzi wa mambo wamekuwa wakidanganyika na madai ya amna hii, na hivyo kusadikisha kisemwacho kuwa haifani kuamini chochote kisichokuwa na dalili kutoka ndani ya Qur’ani, na hivyo kufutilia mbali ushahidi na dalili ya hadithi! 

[2]. Behar Al-Anwaar:42/256.

[3]. Al-Khesaal: Ab’wabul arbai’na, hadithi:19.