KUJIWEKA MBALI NA QUR’ANI NDIO SABABU YA KUFELI WAISLAMU
KUJIWEKA MBALI NA QUR’ANI NDIO SABABU YA KUFELI WAISLAMU
Uchaguzi wa hadithi izungumzayo kunako malalamiko haya haukufanyika bila sababu au kwa fikra za kianasa, bali umetokana na ufahamu na muono wa mbali katika kuuchambua uhalisia wa waislamu na hali waliyofikia, kiasi kwamba wamefikia kuzitoa nafsi zao zikiwa kwenye sahani za dhahabu, kwa maadui wao ambao ni ibilisi na nafsi inayo amrisha maovu, iliyoandaliwa na makafiri wakimagharibi ambayo wanajitahidi wakati wote kuwaondolea waislamu heshima, sharafu na utukufu wao ambao ni kitabu kitakatifu cha Qur’ani, hadi imefikia hatua leo hii Qur’ani imekuwa ngeni kwao، jambo ambalo limesababisha maumivu ya moyo wangu.
Sababu kuu ya kufeli, kudhoofika na kusambaratika Waislamu ni kuipa mgongo kamba ya Mwenyezi Mungu na kutoshikamana nayo, kamba aliyowaamuru kushikamana nayo pale aliposema:
[وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللّهِ جَمِيعاً وَلاَ تَفَرَّقُواْ]
"Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu wala msifarakane"[1], kisha bwana mtume (s.a.w.w) akabainisha makusudio ya kamba hiyo aliposema:
(وإني مخلف فيكم الثقلين: الثقل الأكبر القرآن والثقل الأصغر عترتي أهل بيتي هما حبل الله ممدود بينكم وبين الله عز وجل ما إن تمسكتم به لم تضلوا،. . . الحديث).
"Mimi ni mwenye kukuachieni vizito viwili: kizito kikubwa ni Qur’ani na kizito kidogo ni kizazi na ahlul-bayt wangu, viwili hivyo ndio kamba ya Mwenyezi Mungu baina yenu na Mwenyezi Mungu, iwapo mtashikamana nayo hamtapotea, ...”[2].
[1]. Suurat Aal Imran:103.
[2]. Biharul Anwaar: 92/102.