MALALAMIKO YA QUR’ANI

| |times read : 537
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

MALALAMIKO YA QUR’ANI

Nimekusudia nianze kwa kusoma hadithi ilinukuliwa katika kitabu cha Al-kafi na Al-khiswar kutoka kwa Abu Abdillah (a.s) alisema:

(ثلاثة يشكون إلى الله عز وجل مسجد خراب لا يصلي فيه أهله وعالم بين جهّال ومصحف معلّق قد وقع عليه الغبار لا يُقرأ فيه)

(Vitu vitatu, vitamlalamikia Mwenyezi Mungu:

1.       Msikiti ulioachwa na usio na mtu ajae kusali humo.

2.       Aalimu (msomi) aliye miongoni mwa wasiojua dini, na

3.       Qur’ani tukufu iliyowekwa mahali ambapo hakuna mtu wa kuisoma na ikabakia katika hali ya kujaa mavumbi.)[1]

Na Ahlul bayt wa mtume (a.s), hasahasa imamu wa zama hizi na alieshikilia madaraka kwa sasa (a.t.f) ni mifano iliyo wazi ya aalimu. Hivyo, vitu vitatu vitakavyomlalamikia Mwenyezi Mungu vitakuwa ni: Qur’ani, Ahlul bayt na msikiti, na kuna riwaya nyingine ilipokelewa kutoka kwa bwana mtume (s.a.w.w) ikionyesha maana hii pia, alisema:

(يجيء يوم القيامة ثلاثة يشكون: المصحف والمسجد والعترة يقول المصحف يا ربّ حرّفوني ومزقّوني، ويقول المسجد: يا رب عطلّوني وضيعّوني وتقول العترة يا رب قتلونا وطردونا وشردونا، فأجثو للركبتين في الخصومة فيقول الله عز وجل لي: أنا أولى بذلك منك)

Vitu vitatu siku ya kiyama vitakuja hali ya kuwa vikimlalamikia Mwenyezi Mungu: Qur’ani, msikiti na Ahlul bayt. Qur’ani itasema: Ewe Mola wangu mlezi! Walinipotosha na wakaniacha, na msikiti utasema: Ewe Mola wangu mlezi! Walinifunga na wakanipoteza, kisha Ahlul bayt wanasema: Ewe Mola wetu mlezi! Walituuwa, walitufukuza na walitutimua katika miji yao, kisha nitakaa kwa magoti yangu (ili kutatua) mgogoro, Mwenyezi Mungu ataniambia: Mimi ndiye ninayesitahiki kuliko wewe katika hili”[2].

 

Kutokana na hadithi hii tunajifunza mambo kadhaa:

Jambo la kwanza: hakika misingi inayojenga uma wa kiislamu na mihimili ya uwepo wa jamii ya kiislamu ni haya matatu yaliyotajwa ndio maana yametiliwa manani. Hivyo, kwa msingi huu hadithi hii itakuwa na maana sawa ile hadithi maarufu ya thaqalaini (vizito viwili) isemayo:

(إني تارك فيكم الثقلين كتاب الله وعترتي أهل بيتي ما إن تمسكتم بهما لن تضلوا بعدي أبداً وقد نبأني اللطيف الخبير أنهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض يوم القيامة)

‘‘Mimi ninaacha kati yenu vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi change, ikiwa mtashikamana navyo, kamwe hamtapotea baada yangu, naye mwingi wa huruma aliyemjuzi wa yote amenijulisha kwamba havitotengana kamwe mpaka vitakaponijia kwenye hodhi (ya kauthar) siku ya kiyama’’[3].

       Qur’ani na Ahlulbayt ni viwili kati ya vile vitu vitatu vitakavyomlalamikia Mwenyezi Mungu, na cha tatu ni msikiti ambao ndio sehemu Qur’ani na Ahlulbayt hutekelezea majukumu yao katika jamii kwani vyote huhusiana na uma kupitia nyanja mbalimbali za msikiti.

Jambo la pili: Kuujulisha uma kwamba utapuzia na kuipa mgongo mihimili hii mitatu, hivyo bwana mtume (s.a.w.w) alielezea malalamiko haya ikiwa ndio ukweli na uhalisia uliopo, na hivyo kuutahadharisha uma na msiba huu wa kuipuzia mihiili hii, na akaonyesha adhabu ya jambo hilo na ukubwa wake pale alipofanya Mwenyezi Mungu kuwa ndio mwenye haki yake iliyopotea, na wakati huohuo yeye ndio hakimu mwadilifu.

Na kwakuwa mihimili hii mitatu ndio misingi ya uwepo wa Uislamu, kuipuuza na kuipa mgongo maana yake ni kutoweka kwa Uislamu na kumalizika kabisa. Ndio maana ikiwa ni wajibu wetu kuudurusu kila muhimili kivyake ili kubainisha athari yake katika maisha ya uma wa kiislamu, kuelezea hasara kubwa itokanayo na kuupa mgongo kila muhimili na kuzungumzia njia zitakazoweza kuhuisha nafasi yake chanya katika maisha ya waislamu.

Hivyo, nimeona ni wajibu wangu nijichague ili kuwasilisha malalamiko na mashitaka haya matatu nikianza na lalamiko na shitaka la kizito kikubwa zaidi ambacho ni Qur’ani:

       Qur’ani tukufu ndio kamba iliyonyoshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu hadi kwa waja wake, na yafuatayo ni malalamiko atakayofikisha mtume (s.a.w.w) siku ya kiyama mbele ya Mwenyezi Mungu pale atakaposema: 

[وَقَالَ الرَّسُولُ يَا رَبِّ إِنَّ قَوْمِي اتَّخَذُوا هَذَا الْقُرْآنَ مَهْجُورًا]

‘‘Na mtume alikuwa akisema: Ewe Mola wangu mlezi! Hakika watu wangu wameifanya Qur’ani hii yenyekuhamwa’’[4], na akawatahadharisha waislamu na hatari hii pindi alipowaeleza sababu ya kupotoka kwa umati zilizopita, sababu ambayo ni kuyaacha waliyotelemshiwa na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema:

[قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَسْتُمْ عَلَى شَيْءٍ حَتَّىَ تُقِيمُواْ التَّوْرَاةَ وَالإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ]

‘‘Sema: Enyi watu wa kitabu! Hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu mlezi’’[5]. Hivyo, yeyote atakaye shikamana na yaliteremshwa na Mwenyezi Mungu, kwa hakika atakuwa kafuata njia imfikishayo kwake na atakaye yaacha na kujitenga nao atakuwa ameangamia na kuhiliki.

       Na chanzo cha mashtaka na malalamiko haya ya bwana mtume (s.a.w.w) ni jamii zetu za kiislamu[6] kupuzia usomaji wa Qur’ani, kuipa umuhimu na kutafakari aya zake, achilia mbali kuipa hadhi ya kuongoza katika maisha ili iwe ndio kigezo na muongozo unafuatwa na wenyekutaka kuongoka katika nyanja zote za maisha, mpaka imefikia hatua Qur’ani inasahaulika katika jamii za kiislamu, haikumbukwi isipokuwa kidogo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, hata huko kuikimbuka na kuitilia manani ndani ya mwezi wa Ramadhani, ni kwa sababu ya mahusiano makubwa yaliyopo baina na Qur’ani na mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwani imepokelewa hadithi kutoka kwa bwana mtume (s.a.w.w) kwamba:

   (إن لكل شيء ربيعاً وربيع القرآن شهر رمضان)([7]).

‘‘Hakika kila kitu kina msimu, na msimu wa Qur’ani ni mwezi wa Ramadhani’’[8], lakini hii haimanishi kuipuuza na kuipa mgongo au kupunguza kuisoma ndani miezi mingine.



[1]. Al-kaafi: kitabu fadhlil Qur’an, babu qiraatil Qur’ani fil mushaf, hadithi:3, na Al-khiswal: 1/142 abwabu thalatha.

[2]. Wasailus Shi’a: kitabu salat, abwabu ahkamil masajid, babu:5, hadith:2.

[3] Hadithi hii imenukuliwa na vitabu vya kisuni na vile vya kishia, kwa maelezo zaidi rejea kitabu cha (Almuraja’t) cha Sayyed Abdulhuseini Sharafud Diin Almusawi.

[4]. Surat Al-Furqaan: 30.

[5]. Surat Al-Maidah: 8.

[6] . Nimechunguza idadi kadhaa ya sampuli za watu waliochaguliwa, walikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa mwanzo kukubaliwa katika shule za kidini (hawza za kielimu), ili kujua namna wanavyoipenda Qur’ani, kwani makadirio ni kwamba, hawa ndio wanaoshika nafasi za juu katika ufahamu wa mambo ya dini na katika imani, kiasi kwamba ufahamu na Imani zao zimewasukuma kuchangua njia hii, lakini (lakushangaza) nimekuta baadhi yao hawajawahi kuhitimisha Qur’ani hata mara moja –wakati wao ndio watu wa mimbari-! Na wengine wamehitimisha mara mbili tu maishani mwao! Na wengine husoma sura tofauti totauti wawapo kwenye minasaba ya kidini. Haya ni kwa upande wa kusoma Qur’ani tu, achilia mbali kuifahamu na kuelewa mana ya aya zake na kutafakari juu ya mafunzo na madhumuni yake. Ikiwa upande ule ni shida, basi upande huu kutofahamu kwao ni zaidi.

[7].

[8]. Ma’anil Akhbaar: sheikh Swadooq, uk: 226.