UFUNGUZI

| |times read : 494
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

UFUNGUZI

Watu wamezoea kufungua vikao, mikutano, makongamano, na vipindi vya redio na televisheni kwa kusoma aya za Qur’ani tukufu lengo likiwa ni kutaka baraka na kuzitukuza aya hizo. Ada hii imekuwa ikifanywa hata nawasio kuwa waislam, jambo linaloonyesha haiba ya kitabu hiki katika nyoyo za maadui na wapinzani wake. Basi ni uzuri ulioje na sisi wanahauza (wanafunzi wa masomo ya dini) tukawa tukifungua masomo yetu kwa Qur’ani tukufu, na yapaswa ufunguzi wetu uwe wenye ufahamu na unaoendana na roho ya Qur’ani, madhumuni na maana zake, na usiwe ni ufunguzi wa kimaoyesho, mfano wa nyimbo na kaswida za kidini au ikiwa ni mfano wa kinga na hirizi.