Marjii Ayatollah Yaaqubi, ahimiza jamii kuharakia katika swala la kujitolea

| |times read : 603
Marjii Ayatollah Yaaqubi, ahimiza jamii kuharakia katika swala la kujitolea
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Marjii Ayatollah Yaaqubi, ahimiza jamii kuharakia katika swala la kujitolea

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Marjii ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqubiy amehimiza mno kuwepo kwa misingi ya kijamii ni kuwekeza zaidi katika kujitolea katika hali ambayo kutajitokeza upungufu kutoka serikalini katika kutekeleza majukumu yake kupitia mashirika yenye jukumu la kufuatilia haja na dharura za wananchi, kama vile mashirika ya afya, elimu, mipango miji na mengineyo ili tu kuweza kuziba zile nafasi ambazo zitaonekana na ambazo zinaakisi moja kwa moja maisha ya kila siku ya wananchi.

Hayo yamekuja baada ya ujumbe maalumu kutoka idara mbali mbali za mashule mjini Najaf kumtembelea Ayatollah Yaaqubiy ikiwa ni pamoja na kutoa shukrani zao kwa ushirikiao mzuri kutoka katika ofisi ya Ayatollah Yaqoobiy hasa katika maswala ya kujenga na kuboresha au kukamilisha baadhi ya haja za mashule hayo ikiwa ni katika kufanyia kazi kauli ya uharaka wa kuchuma elimu katika mkoa huo.

Pia katika kikao hicho Ayatollah ameomba wanancho wote kuwa bega kwa bega kwa mustawa wa moja mmoja au hata jamii kwa ujumla kueneza utamaduni wa kwamba “...Kila mmoja wenu ni kiongozi” katika kusaidiana na kusimamia baadhi ya mambo ya wao kwa wao hasa wale wasiojiweza katika wao na kuacha kabisa kutegemea msaada wa serikali  ambao kwa namna moja au nyingine umeonekana kutokidhi mahitaji.

Kama ambavyo ametia tahadhari katika kutochukulia umuhimu wadhaifu, na kutowahi katika kuwasaidia, kwani jambo hili litapelekea kutokuwepo kwa uwiano katika jamii na mwisho wa siku kuangukia kuwa ni jamii iliyokufa, Mwenyezi Mungu atuepushe.

Pia Ayatollah alikuwa na baadhi ya mambo ambayo kwa mujibu wa haja na matakwa ya jamii husika:

1.   Umuhimu wa maktaba ya mjini Mousil

2.   Umuhimu wa kugawa vitabu kwa wanafunzi, na kisha kujaribu kuimarisha mashule na kuyaweka katika mazingira mazuri.

3.   Kujaribu kujenga sehemu za mayatima na kukidhi mahitaji yao.