Haifai wazazi kuchunguza vifaa vya watoto wao.

| |times read : 43
Haifai wazazi kuchunguza vifaa vya watoto wao.
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Haifai wazazi kuchunguza vifaa vya watoto wao.

 Kwa mujibu wa Sheikh Muhammad Yaaqubiy ni kwamba haifai kwa wazazi na wenye mamlaka kuchunguza vifaa vya watoto wao kama vile simu, kompyuta mpakato na vifaa vingine vya kisasa kwa hoja ya kwamba wanawachunga kunako kuangukia haramu.

Sh Yaaqubiy ametoa hoja ya kwamba jambo hili ni kuvunja amri ya Mungu aliposema “...Wala msichunguzane..”[1]. na kwamba lengo linaweza kuwa sahihi lakini pia liwe ni kwa njia zenye kufaa (Lengo halihalalishi kila njia) hasa pale inapokuwa si sahihi na halali. Na mama na baba kuna wakati kutokana na kuchunguza kwao huku wanagundua baadhi ya makosa na wanayatibu, ila wakati mwingine ni kwamba wazazi hawa wanashindwa kutibu na mwisho wake hupoteza kabisa imani zao kwa watoto wao, na wao wanakosa ule utayari wa watoto kufunguka kwao matatizo yao, na hii i hatua mbaya zaidi katika mahusiano baina ya wazazi na watoto wao.

Hivyo ni muhimu kuwafuatilia watoto kwa umakini na werevu mkubwa mno, bila ya kuingilia uhuru wao.

Pia Sheikh katika hili hakusahau nafasi ya wazazi katika kuwaelekeza watoto wao baadhi ya mambo ambayo yanawatia shaka wazazi hao, kama vitendo vya watoto hao kujifungia peke yao chumbani na kuongea baadhi ya mambo mabaya na mfano wake, hivyo wazazi katika hili wanatakiw akuchukua hatua za tahadhari.

Na hukumu hii pia inahusika kwa mke na mume, haifai kwao kuchunguzana kwa yake ambayo kila moja wao anashakia, kwani kama tulivyosema jambo hili linaweza kupelekea kupotezeana imani na hali ya kufungukiana ya moyoni.

                                                        Ayatollah Mohammad Yaaqubiy[1] Surat Hujurat aya 12