Hotuba za sala ya Eidul Adh-ha mwaka 1439

| |times read : 794
Hotuba za sala ya Eidul Adh-ha mwaka 1439
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Hotuba za sala ya Eidul Adh-ha mwaka 1439

Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqubiy.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu

Ofisi ya Ayatollah Muhammad Yaaqubiy Mjini Najaf, ilifanikiwa kuandaa ibada ya Eidul Adh-ha ambayo ilihudhuriwa na umati wa watu  na ambapo Ayatollah Yaaqubiy alitoa hutuba zote mbili kuwahutubia wahudhuriaji wa ibada hiyo.

Katika hotuba ya kwanza alitanguliza aya ya Mwenyezi Mungu isemayo “....Na kwa hakika mwanadamu amekuwa ni mwingi wa pupa...”[1]

Na kisha kuweka wazi kuwa katika kila pupa kuna majuto, isipokuwa pupa ya kufanya mambo mema.

Kadhalika katika hotuba ya pili aliweza kutoa somo kutoka katika riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Imamu Sajjad (as).

Katika Hotuba ya kwanza Ayatollah Yaaqubiy alielezea baadhi ya sifa na hulka za mwanadamu ambazo zimetajwa ndani ya Quran tukufu kama vile pupa “...Kwa hakika mwanadamu ameumbwa katika hali ya pupa...”[2]

Dhulma na Ujinga “...Na akayakubali mwanadamu, kwa hakika yeye ni Mwenye kudhulumu na mjinga pia...”[3]

Na sifa nyinginezo ambazo Quran imezitaja kuhusu mwanadamu.

Ayatollah katika kuelezea aya hizi amesema kuwa lengo na makusudio yake si kwamba asili ya mwandamu ndio inayosifika na sifa hizi, asili ambayo Mwenyezi Mungu ameiumba katika umbo lililokamilika kabisa. “...Kwa hakika tumemuumba mwanadamu katika umbo lililokamilika...”[4] Bali makusudio ya aya hizi ni ule upande wa kimatendo wa mwanadamu, kwa sababu katika upande huu mwanadamu anaweza akaacha kuhifadhi usalama wa maumbile yake au kushikamana na yale ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa anayataka, bali yeye akafuata matamanio yake na ambayo yanamuhadaa huku shetani naye akijaribu kumpambia matendo yake mabaya hayo.

Aidha katika hotuba yake hiyo ya kwanza Ayatollah Yaaqubiy alitilia mkazo moja ya sifa ambazo mwanadamu anasifika nazo ni sifa ya pupa na kutokuwa na subira na uvumilivu katika kuchukua maamuzi. Kiasi kwamba anakurupuka na kujiingiza katika madhara. “....Kwa hakika mwanadamu ameumbwa na pupa, nami nitawaonyesha alama zangu wala msiwe na pupa...”[5]

Katika kubainisha zaidi kunako hilo Ayatollah akasema

 “....Ni lazima mwanadamu awe na subira na ubimilivu katika kufikia malengo yake, pia achunge sheria na usafi wake katika kuyafikia, kwani imepokelea kutoka kwa Mtume Muhammad (saww) kwamba kwa hakika watu wameangamizwa na pupa, na laiti watu wangalitulia basi asingaliangamia hata mmoja wenu...”

Pia akaja na baadhi ya mifano ya pupa ambayo imekemewa ambayo ni kama:

·       Mwenye kutaka utajiri wake uongezeke na akajikuta anatumia njia za hiyana na wizi pamoja na kuchukua mali za watu na mfano wake, au mifano mingine ni kama vile vijana ambao wanakuwa na pupa ya kuanzisha mahusiano ya kimapenzi nje ya misingi ya kisheria na dini, kiasi kwamba mwanamke anjikuta katika mtego na mwisho wa siku anadanganywa na kuachwa. Au kama vile baadhi ya watu ambao huvamia miamala ya watu kwa ajili ya kuwawekea ugumu, kiasi kwamba kama angeamiliana naye kwa upole basi huenda ingekuwa ni njia ya kumwepusha na baadhi ya mambo ya haramu.

 

Ama katika hotuba yake ya pili Ayatollah Yaaqubiy alichukua hotuba ya Imamu Sajjad kama mwongozo wa mazungumzo yake. “...Ewe Mwenyezi Mungu, nijaalie nguvu ya kuisahau dunia yenye kudanganya, na kuwa na moyo wa kuambatana na nyumba ya milele, nijaalie nguvu ya kujiandaa kabla ya kufikwa na mauti...”

Kisha katika maneno yake akataja baadhi ya riwaya zenye kuhimiza jambo la kujiandaa na mauti, miongoni mwake ni riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Imamu Ally (as) akisema:

“...Hakika mwenye akili inatakiwa awe katika tahadhari kunako mauti, na ajiandae kwa wema kabla ya kuelekea katika makazi ambayo mtu atatamani kifo kimchukue lakini haitakuwa hivyo....”.

Kama ambavyo pia Ayatollah alitaja baadhi ya aya tukufu zenye kuelezea kwamba swala la mauti na kujiandaa kuyaelekea, na kutokuwa na hofu ya kukutana nayo ni moja ya alama za imani na kupenda kukutaa na Mwenyezi Mungu (swt). Kwani Mwenyezi Mungu katika Quran anasema “...Sema kuwaambia, enyi Wayahudi, ikiwa mnadai kuwa nyie ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasi na wengine basi tamanini kifo ikiwa mnasema ukweli...”[6]

Kama ambavyo Yatollah katika maelezo yake alielezea namna ya kujiandaa kukielekea kifo, ikiwa ni kutaja baadhi ya riwaya ambazo zimetajwa na vitabu vya Akhlaq (adabu) kwa kutaja baadhi ya vipengele vyake tofauti tofauti kwa mujibu wa hatua ambazo mwanadamu atazipitia katika safari yake hiyo ya kuelekea akhera. Mfano ni riwaya iliyopokelewa kwamba siku moja alikuja mtu mmoja kwa mtume Muhammad (saww) na kwamba mbia kuwa anatamani kifo. Inapokelewa kwamba siku moja kuna mtu alikuja kwa Mtukufu Mtume Muhammad (saww) na kumwambia “...Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unanipa ruhusa na ni vizuri kutamani kifo..”.

Mtume akamwambia

“....Kifo ni jambo ambalo kila mmoja wetu hana budi kulifikia, pia ni safari ndefu mno ambayo kila mwenye kutaka kuiendea basi hana budi ya kubeba zawadi kumi. Zawadi kwa Isarel (malaika mtoa roho), zawadi ya kaburi, zawadi ya munkir na nakir (malaika wa kaburini wenye kuhusika na kuuliza maswali), zawadi kwa ajili ya mzani wa matendo, zawadi kwa ajili ya Sirat (njia ambyo kila mmoja atatakiwa kupita kama mchujo), zawadi ya Malik, zawadi ya Ridhwan, zawadi ya Mtume, zawadi ya Jibril na zawadi ya Mwenyezi Mungu (swt).

Ama kuhusu zawadi ya Israel ni mambo manne, kuridhia na kujishusha mbele ya wapinzani, kusahau na kuacha yaliyopita, kutamani kukutana na Mwenyezi Mungu, na kutamani kifo chenyewe.

Na ama zawadi ya za kaburi ni mambo manne, kuacha umbea, kujisafisha vizuri baada ya kutoa haja ndogo (istibraa), kusoma Quran na kusali sala za usiku.

Na ama zawadi za Munkiri na Nakir ni mambo manne, kuwa mkweli katika manenno, kuacha kusengenya, kukubaliana na haki, kuwa mnyenyekevu kwa kila mmoja.

Ama zawadi za mzani wa matendo i mambo manne, kuwa na moyo mkunjufu, uchamungu wa kweli, kuwa karibu na kutembea na wengine na kuwa mwenpesi na mwenye kudumu katika kuomba msamaha.

Na zawadi za Sirat ni mambo manne, kuwa ni nia thabiti katika matendo, kuwa natabia nzuri, kuzidisha kumtaja Mwenyezi Mungu, na kuvumilia maudhi.

Ama zawadi za Malik ni nne, kulia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kutoa sadaka kwa siri, kuacha maasi, na kuwafanyia wema wazazi wawili.

Na ama zawadi za Ridhwan ni mambo manne, kusubiri katika maudhi, kushukuru wakati wa neema, kutoa mali zako kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kuhifadhi amana katika mali za umma.

Na zawadi za Mtume ni mambo manne, kumpenda, kufuata sunna zake, kuwapenda watu wa nyumba yake, kuulinda ulimi kutokana na maovu.

Ama zawadi za jibril ni mambo manne, kupunguza kula, kupunguza kulala, kudumisha kumsifu Mungu, na kupunguza maneno.

Na zawadi za Mwenyezi Mungu ni mambo manne, kuamrisha mema, kukataza mabaya, kutoa nasaha kwa viumbe, na kuwaonea huruma watu wote....”.

 

Na baada ya hotuba mbili Ayatollah aliweza kupeana mkono wa heri na pongezi za Eid na waumini na wote waliohudhuria katika sala hiyo.

 



[1] Surat Israa aya 11

[2] Surat maarij aya 19

[3] Surat Ahzab aya 72

[4] Surat Tiin ay 4

[5] Surat Anbiya aya 37

[6] Surat Jumua aya 6