Uislamu ndio muasisi na kiongozi wa utamaduni na usuluhishi kwa muda wote.

| |times read : 627
Uislamu ndio muasisi na kiongozi wa utamaduni na usuluhishi kwa muda wote.
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema na mwenye kurehemu

Uislamu ndio muasisi na kiongozi wa utamaduni na usuluhishi kwa muda wote.

Kiongozi Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqubiy aliweza kupata ugeni wa mtafiti wa Kifaransa Bw Gilles Kepel kutokea chuo kikuu cha siasa mjini Paris Ufaransa ambaye ni mtafiti wa maswala mbalimbali hasa yanayohusiana na vikundi vua Kiislamu vyenye lengo la kuondoa tofauti.

Kwa upande wake mtafiti huyo alipendekeza kumzuru kiongozi huyu wa kidini na kufanya katika mambo yake ya kwanza kabisa baada tu ya kuingia mjini Najaf, ikiwa ni katika kutaka ushauri pamoja na rai yake juu ya mustakabali wa maeneo a Kiislamu katika kukabiliana na ugaidi pamoja na kutengana, mambo ambayo yamedhihirika katika miaka ya karibuni na ambayo yamekuwa ni kizuizi kikubwa katika kufanikisha na kuhakikisha harakati za Kiislamu.

Aidha Bw Kepel alitaka kujua misingi na mchango wa Cheo ch Umarji katika kukabiliana na changamoto hasa katika kuijenga Iraq mpya.

Katika kujibu maswali ya Bw Kepe, na kubainisha baadhi ya misingi ambayo madrasa ya watu wa nyumba ya Mtume Muhammad saww, Ayatollah Yaaqubiy aliweka wazi kwamba misingi ya madhehebu ya Kishia kwanza halijasimamia tu katika swala zima la kuheshimu utu, bali hata wasiokuwa wanadamu pia wamewekwa katika misingi hiyo.

Kwani tuna hadithi Qudsi ambayo Mwenyezi Mungu ansema “Viumbe wote ni familia yangu, na nampenda zaidi mwenye kuipenda familia yangu...” ambapo neno kiumbe hapa halimaanishi tu mwanadamu, bali hata viumbe wengine pia.

Au hadithi Qudsi nyingine ambayo Mwenyezi mungu anasema kuwa Muumini ana heshima kubwa kuliko hata Kaaba.

Hivyo Uislamu kwa mujibu wa misingi ya Kishia ni kwamba umesimamia katika kuheshimu haki za watu, ikiwa i pamoja na kueneza usawa, kusamehe na amani. Kama ambavyo pia ukiangalia utakuta kwamba kuna jambo zaidi ya hayo, jambo la kuamiliana kwa mapenzi na upendo baina yetu. Kuna hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq yenye kusema

“...Na je, kuna dini zaidi ya upendo..”[1]

Kama ambavyo Ayatollah ameweka wazi kuwa Uislamu hutegemea zaidi njia ya diplomasia kama njia kuu ya kutatua mizozo na ugomvi, na hayo tumeyaona katika historia ya Mtume pamoja na Maimamu (as). Unakuta Imamu Ally as pamoja na kuwa ni kiongozi ambaye watu waote wamekubaliana kuongozwa naye anasisitiza mno swala la kutomwaga damu, huku akitumia muda wake mwingi sana kumpa usia Muawiya juu ya umuhimu wa jambo hili kabla ya kuingia naye vitani. (pamoja na kwamba Muawiya hakuwa ni mwenye kufanyia kazi usia huo).

Pia unakuta kwamba Imamu alituma ujumbe kupitia ndugu yake Abdullah Bin Abbas kwenda kwa Khawarij, ambapo kupitia njia hiyo kuna zaidi ya watu 6000 waliweza kuongoka na kurejea katika njia ya haki.

Aidha pia Sheikh Yaaqubiy ameashiria katika mazungumzo yake kunako mifano hai tuliyonayo katika zama zetu hizi, na kuashiria kunako wito wake wenye kulenga kutotengana kifikra wala kidini, kupinga ugaidi kwa kujaribu kukata mizizi na asili ya vikundi hivi kwa kufungua mlango wa mazungumzo ambayo yanaweza kufikia natija nzuri na tatuzi.

Kwa maana watu wengi wenye kukengeuka huwa wana matatizo ya kifikra ambayo huwapeleka moja kwa moja kuingia katika kutumia nguvu kabla ya kuangalia njia ya mazungumzo inaweza kufikisha wapi, kutokana tu na kuharibiwa fikra zao.

Pia Ayatollah ametumia nafasi hiyo kuwaomba ndugu zetu Ahlu Sunna kuacha wazi mlango wa Ijtihad ambao umefunga tangu zama za Maimamu, ili tu kuweza kutoa nafasi kwa watu kusoma zaidi na kujiepusha na utoaji fatwa za juu juu, na ikiwezekana swala la fatwa liwe ni maalumu kwa watu wenye uelewa wa kielimu na adabu, mambo ambayo ndio masharti makubwa ya ngazi hiyo ya Ijtihadi (Ngazi ya juu kabisa katika elimu ya dini, kiasi kwamba mtu anakuwa na uwezo wa kutoa hukumu za kisheria kutoka katika machimbuko yake kama vile Quran, Suna nk).

Pia katika nukta hiyo kuhusu hawa Marajii na viongozi wa juu, Ayatollah ameashiria umuhimu wa wao  kuwa na hali ya kuhifadhi umoja na maslahi ya umma pamoja na kuwalingania kunako yenye kuwajenga. Pia kuwejengea hali ya kupenda nchi zao, jambo ambalo tayari unaweza kuliona kwa baadhi ya wananchi kuelekea mambo yenye kutaka kuharibu nchi zao, pamoja tofauti zao kiimani na kimadhehebu.

Pia Ayatollah Yaaqubiy ametoa ushauri wake kwamba viongozi wa dini pamoja na kutakiwa kuwa na hali ya kuhisi majukumu yao kwa raia, bado hawatakiwi  kujikita zaidi katika mambo ya Kisiasa, kwani si katika mambo yao, na hata kama wataingilia basi iwe ni katika kutetea na ulinda maslahi ya watu, kama vile katika nukta hatari kama kupambana na uwepo wa Daesh nchini Iraq na kwingineko.

Kama ambavyo pia Sheikh Yaaqubiy ameweka wazi namna ambavyo anapambana na baadhi ya majaribio yenye kulenga kutenganisha baina ya nidhamu za kimiji na nidhamu za Kiislamu, kwa kueleza kwamba Uislamu ndio muasisi na chanzo cha hizo nidhamu za kimiji katika sehemu za Arabu, kama ambavyo Uislamu ndio chanzo na kiongozi wa Uatamaduni wa kibinadamu katika zama zote.

Kwa maana kwa kila mwenye kufuatilia maisha ya Waarabu kabla ya Uislamu, hakuti mbali na kuwa walikuwa ni watu wenye kutengana na wasio na utamaduni, lakini kwa baraka za Uislamu waliweza kuwa jamii yenye tamaduni na yenye kukaa pamoja.

Kama ambavyo pia Sheikh ameweka wazi kwamba hata hiyo misingi ya kibinadamu ambayo leo hii nchi za Kimgharibi zinajivunia nayo, asili yake hasa ni katika Uislamu, na hali ya Waislamu kuwa nyuma katika tamaduni ni kutokana na kuachana kwao na kufuata misingi hiyo ya Uislamu mtukufu. Kwa maana Uislamu ni dini ambayo imekuja kwa lengo la kujenga, kulinda na hata kuzipa nafsi mambo yenye kuwafikisha katika ukamilifu pamoja na kujenga miji na tamaduni zake.

Mwisho kabisa mgeni wa Sheikh alipata nafasi ya kutoa shukrani zake hasa kwa Sheikh Yaaqubiy kwa kuweza kumkaribisha kwa moyo mkunjufu, na kwa yote ambayo ameweza kuzungumza naye.

Haya yote yalitokea mbele ya wageni wengine wakubwa kama vile ujumbe kutokea Wizara ya mambo ya nje ya Iraq ambao wao ndio walipanga ujio wa mgeni huyu.

 

 



[1] Alkhiswal  21/74