Marjii Ayatollah Yaaqubi, ahimiza umuhimu wa kutambua vipawa na kuvitukuza

| |times read : 501
Marjii Ayatollah Yaaqubi, ahimiza umuhimu wa kutambua vipawa na kuvitukuza
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Marjii Ayatollah Yaaqubi, ahimiza umuhimu wa kutambua vipawa na kuvitukuza

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu

Kiongozi wa Juu wa Kidini, Ayatollah Shekh Muhammad Yaaqubiy amezitaka na kuzihimiza mamlaka za ndani kuongeza kutilia umuhimu zaidi katika kutambua na kuvipa thamani vipawa katika nyanja tofauti tofauti, zikiwemo nyanja za michezo, ikiwa ni pamoja na kuandaa mazingira ya kufaulu katika nyanja hiyo.

Hayo ameyaeleza pindi alipokutana na mabingwa wa michezo ya nguvu kwa watu wasiojiweza walipomtembelea katika ofisi yake mjini Najaf Asharaf.[1]

Pia Ayatollah Yaaqubiy ametumia nafasi hiyo kuwashukuru na kuwatukuza mabingwa wote wa nchi, pamoja na walimu wao ambao wanatumia muda wao katika kuwaandaa pamoja na kuwepo kwa mazingira magumu na ufinyu wa vifaa, kama ambavyo pia Ayatollah Yaaqobiy ameonyesha namna alivyofurahishwa na ushindi huo ambao umepelekea kupatikana kwa medali za dhahabu na kuifanya nchi kwa ujumla kung’aa katika anga za kimataifa.

Ikumbukwe pia kuwa Ayatollah Yaaqubiy alishawahi kuashira katika hotuba zake mbalimbali kuhusu ujumbe muhimu sana ambao unaweza kubebwa na wanamichezo na kuufikisha maeneno mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuunganisha umma wa Iraq pamoja na kuwapa heshima, jambo ambalo wanasiasa wengi wa kileo wameshindwa kulifanya na kulitimiza.

 

 

Jumamosi 8 Jumadal Akhar 1437

19/3/2016



[1] Mabingwa hao ambao ni Jarrah Nasar na ahmad Gina, walipata ushindi wa juu na kutunukiwa medali katika mahfali mbalimbali za nchi ikiwemo na kupata nafasi ya kuelekea nchini Brazil mwaka 2016