“Hisia zina nafasi kubwa ya kuunganisha wanadamu” Marjii Ayatollah Yaaqubi.

| |times read : 500
“Hisia zina nafasi kubwa ya kuunganisha wanadamu”  Marjii Ayatollah Yaaqubi.
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

 “Hisia zina nafasi kubwa ya kuunganisha wanadamu”  Marjii Ayatollah Yaaqubi.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu

Kwa kupitia baadhi ya mambo yaliyotokea katika masiku yaliyopita,  yameweza kuonyesha kwamba wanadamu kuachilia mbali dini zao, mataifa yao, jografia yao na hata jamii zao, bado wana sehemu kubwa mno ambayo wanashirikiana kitamaduni na tabia za kibinadamu. Tabia ambazo zinarejea katika maumbile asili ya binadamu sahihi. “...Maumbile ambayo Mwenyezi Mungu amewaumba wanadamu kwayo...”[1]

Pamoja na kwamba maumbile haya yanweza kukumbana na sababu za nje ambazo zinakuja kuchafua au hata kuyabadilisha.

Moja ya matukio yaliyotuonyesha hili ni:

·       Kitendo cha wachezaji wa Real Madrid kuvaa vitambaa vyeusi katika mchezo wao, kama ishara ya kukumbuka shambulio lililotokea mjini Balad masiku kadhaa nyuma, ambayo yalihusisha uvamiaji katika moja ya sehemu za kahawa na kuacha athari ya mauaji pamoja na majeruhi kadhaa.  Tena huku kukiwa na maandishi ya lugha za Kiarabu na Kingereza yaliyokuwa yakionyeshwa vizuri na luninga. Na kitendo cha wachezaji na watazamaji kusimama na kukaa kimya kwa muda wa dakika moja kwa ajili ya kuhuzunika na kuungana na wahanga wa tukio hilo na kuwapa pole familia zao.

·       Kitendo cha nchi ya Uingereza  kubadili tarehe za mitihani yake mpaka mwisho wa mwaka kutokana na kuoana na masiku ya mwezi wa Ramadhani, ili tu kuweza kuwapa nafasi wanafunzi wa Kiislamu katika mashule husika.

Haya ni baadhi tu ya matukio, na kabla ya hapo kuna mengine mengi mno ambayo yanaashira kutoa umuhimu kwa majanga na kuungana na wahanga wa vita, ufukara na maradhi. Au hata yanayotokea ulimwenguni katika kuhifadhi mazingira na watu pamoja na haki zao.

Haya yote yanawataka maulama pamoja na wana fikra kuweza kuongeza juhudi zao katika kukuza na kuthamini haya matukio ambayo yanaunganisha watu, na kuwafanya wapendane na kuondoa kila aina ya dhulma, uadui na chuki. Na hii ndio njia bora zaidi katika kuweka watu karibu na kusimika uadilifu, maisha ya furaha na amani kwa watu wa jamii zote.

Ofisi ya Ayatollah Muhammad Yaaqubiy

Alkhamis 11 Shaaban 1437

15/5/2016

 



[1] Surat Rum aya 30