Arobaini ya faraja

Arobaini ya faraja
Imepokelewa kutoka kwa Imamu Sadiq (as) amesema
“........Baada ya kuwa mateso yameshamili kwa wana wa Israel, waliamua kupiga mayowe na kumlilia Mwenyezi Mungu kwa siku 40, hivyo Mwenyezi Mungu akatuma ujumbe kwa Nabii Mussa na Haruna kunako kuwakomboa kutoka kwa Firauni na ikawachukua muda, hivi ndivyo ambavyo nanyi mkifanya Mwenyezi Mungu atawapatia faraja kutoka kwetu, lakini kama hamtafanya hivyo basi itakuwa ndio mwishi wa mambo......”[1]
Hivyo basi sisi tuna nafasi ya kuandaa na kuharakisha faraja na ushindi na mazingira ya kutawala Imamu wa zama, kama ambavyo sisi pia ni sababu ya kutimia hayo. Na hapa Imamu Sadiq anatulingania katika kusimamia majukumu yetu ya kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa maombi na unyenyekevu ili aweze kutengeneza yaliyo haribika katika mambo yetu, kwa kuharakisha ujio wake na utawala wa Imamu ambao utakuja kusambaza uongofu, usawa na uadilifu baina ya watu, kisha kuwatoa katika dhulma na uonevu na uadui. Na kama hatutofanya hivi basi hukumu itakuwa sawa kwetu na kwao kama ilivyo, kama ambavyo hakutakuwa na mabadiliko yeyote bora, na sisi ndio tutakuwa wenye kubeba mzigo huo, pia wao watakuwa ni wenye kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (swt) tu.
Hivyo basi, masiku haya ya arobaini hasa kuanzia Ashura mpaka kufikia arobaini yenyewe, ndio masiku munasibu mno kwa ajili ya kumlilia Mwenyezi Mungu, na hii ni kutokana na kadhia ya Imamu Hussein (as) kuambatana na maswala ya uadilifu, kama ambavyo ni ufunguo na chanzo cha kila nguvu kwa wenye kutaka kuongoa na kutengeneza.
Na naimani kwamba wito huu unastahiki kujibiwa kutokana na mamilioni ya watu kuelekea kuzuru kaburi tukufu la Imamu Hussein pamoja na kuweka vikao maalumu vya kudumisha utajo wake, na kama ambavyo dua huwa ni zenye kujibiwa sana hasa chini ya kaburi la Imamu (as).
Pia mkusanyiko huu wa mamilioni ya watu ni ishara ya imani na alama ya vile “..viungo vyenye kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa utiifu..”[2], na kujiweka makini katika kumuomba msamaha, tena katika sehemu, muda tukufu. hivyo una kila sababu ya kustahiki majibu.
Pia ni lazima tutambue kwamba kutikisa ulimi peke yake kwa dua na maombi haitoshi, bila ya kuwa na ukweli, Ikhlas na kujibadili kuanzia ndani kwa kuweka azma ya kutengeneza watu mmoja mmoja mpaka kuifikia jamii, kama ambavyo Mtume (saww) alisema:
“....Basi mwombeni mola wenu kwa nia safi na za kweli aweze kuwapa tawfiq..”.[3]
Ayatollah Mohammad Yaaqubiy
Najaf Ashraf
9 Muharram 1441
9/9/2019