Dumisheni swala la kupenda nchi yenu katika nyoyo na akili zenu

| |times read : 784
Dumisheni swala la kupenda nchi yenu katika nyoyo na akili zenu
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

 Dumisheni swala la kupenda nchi yenu katika nyoyo na akili zenu

Ayatollah  Sheikh Mohammad Yaaqubiy katika mkutano wake na kundi la wanafunzi na vijana amesema:

Lazima tuwe makini sana na kila aina ya majaribio yenye kulenga kutuondolea hali ya kupenda mji wetu,  kwa kujaribu tu kuelekea katika mambo ya kidini, au vikundi au nasaba au maeneo husika na hata familia, na mengineyo mengi ambayo yanalenga kufuta kabisa upendo wa nchi yetu na kuwashughulisha vijana na haya machafuko yanayoendelea au kuwagawa na kuwatawanya. Jambo ambalo ni njia ya kuweza kutoa nafasi ya kuweza kututawala  na kufanikisha malengo ya hawa viongozi wa vita hii ambao wapo katika kutumikia malengo ya wakubwa wao.

Sawa sisi ni watu wenye dini, lakini kuegemea madhehebu au dini fulani sidhani kama ni kizuizi cha kuweza kupenda na kuegemea pia nchi yetu, na hii ni kwasababu dini haitimii ila kwa uwepo wa nchi ambayo itaieneza na kuandaa yale yote yanayohitajika katika kuieneza na kuilinda. Chukua mfano wa Uislamu mwanzoni kabisa, laiti kama isingalikuwa na dola basi kusingalikuwa na Waislamu ila wenye kutawanyika na dhaifu wenye kuadhibiwa na kukandamizwa. Mwenyezi Mungu anasema :.

“..Mnaogopa watu wasije kuwavamia, Mwenyezi Mungu akawapa hifadhi na kuwapatia ushindi wake kama njia ya kuwaunga mkono...” (surat Anfal aya 26).

Lakini baada ya Mtume kuhamia Yathrib na kuwa ni mji wake (Madina), Uislamu uliweza kusimamisha dola na kutanua mipaka na wigo wake katika bara lote la Arabu, na kisha tukaona namna gani ilivyoweza kuenea ardhini kote kuanzia Mashariki mpaka Magharibi. Hivyo kuweka mbele nchi na kuipenda hakupingani kabisa na kuiweka mbele na kuipenda dini, bali ndio kwanza inaitukuza na kuifanya thabiti. Na pia katika nukta hii kuna idadi kubwa ya riwaya zilizopokelewa, mfano imepokelewa kutoka kwa Imamu Ally (as) kwamba amesema:

“...Kwa hakika miji imesimama kwa watu kupenda nchi zao...”[1]

Na pia imepokelewa tena kutoka kwake akisema:

“....Katika alama za utukufu wa mtu, na mapenzi yake kwa mji na nchi yake...”[2]

Na pia imepokelewa akisema :

“....Kupenda mji ni katika Imani....”[3]

Tazama namna gani watu wasiokuwa na miji wanavyopotelea katika miji ya wengine, jambo linalopelekea kupoteza uhakika na uhalisia wao, na taratibu kujikuta katika hali ya kujivua maumbile yao ya asili na taratibu kutokwa na hali ya kupenda na kutumikia nchi na miji yao.

Ikiwa hali hii ya kupenda sehemu yako inapatikana kwa mnyama ambaye hana hata akili, vipi kwa mwanadamu ambaye ana akili na upeo?. Kwa mfano tunaambiwa kwamba kuna samaki ambao wanaishi katika maeneo fulani, ambapo husafiri kwenda mbali na kuzaliana huko, lakini mwisho wa siku watoto wake hurejea katika mji na sehemu yao ya asili kwa njia ile ile ambayo walipita wazazi wao, pamoja na kwamba hawajawahi hata kuona sehemu hiyo au kuwaona hata wazazi wao walifanya nini.

Nanukuliwa kisa kwamba kuna aina fulani ya mbegu ambazo huwa ni chakula che ndege, na hupatikana katika mji fulani tu. Na bei ya mbegu hizo ni karibuni Dinari 1000 kwa kilo moja. Sasa kuna baadhi ya wafanya biashara waliweza kugundua aina nyingine yenye kufanana na mbegu zile ambayo hupatikana katika miji mingine, hivyo wakawa wanaingiza katika mji ule ambao zile za asili zinapatikana na kujaribu kuziuza kwa bei ya juu ili kupata faida maradufu. Cha ajabu baada ya watu kununua na kwenda kuwapa ndege wao mbegu hizo, hawakuweza kula na kwamba walikuwa wamezoea kula zile tu ambazo zilikuwa ni za asili na za mji ule.

Katika hekaya hii nimeweza kuchukua funzo kubwa mno la kupenda na kuthamini mji wako, ikiwa ni pamoja na kuutendea wema pamoja na watu wake pia, hivyo wakuu wa miji ambao wamefikia hatua ya kubadili hata uraia waweze kutambua kuwa wamebadili jambo ambalo ni ghali kwa ambalo ni duni, na pia hawakuwa ni wenye kuuhini mji wao.

Jumatano 26 Dhulhijja 1437

28/9/2016



[1]                 Tuhaful Uqul 207 pia Biharul QAnwar 45/75

[2] Kanzul Fawaid cha Karaajiy ukurasa wa 34. Pia Biharul Nawar 71/264

[3] Amalul Aamal 1/11. Pia Anwarul Nuumaniyah Juz 2 ukurasa 170.