Maisha yake

| |times read : 1257
Maisha yake
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Maisha yake

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na kurehemu.

Sheikh Muhammad bin Sheikh Mussa bin Sheikh Muhammad Ally bin Sheikh Yaaqubiy bin Alhajj Jaafar.

Alizaliwa katika mji mtukufu wa Najaf mnamo mwezi wa September mwaka 1960, kutoka katika familia yenye kushikamana na dini na maarufu kwa mambo ya uhadhiri na kushikamana na adabu. Na ndio maana kuna baadhi ya wanafamilia hao wamewekwa katika orodha ya watu wenye uwezo mkubwa wa kuhubiri, kama vile baba yake Sheikh Mussa, ambaye ni muasisi wa jarida maarufu la Al Iman. Pia babu yake Sheikh Muhammad Ally maarufu kwa jina la “Sheikhul Khutwabaa” kwa maana ya “Shekhe wa wahubiri”. Pia babu yake upande wa mama yake Sheikh Mahdi, au Babu yake upande wa baba ambaye alikulia katika madrasa na shule za elimu ya Irfani (Kumtambua Mungu), pamoja na adabu, shule ambazo zilikuwa zikimilikiwa na wanazuoni kama vile Marhum Sheikh Jaafar Al Shushtary na Marhum Sheikh Hussein Qulliy Hamadaniy.

Kutokana na baba yake kuwa mashughuli zaidi na harakati na maswala ya kidini pamoja na siasa, pamoja na marhum Sayyid Muhsin Hakim (ambae kwa kipindi hicho ndio alikuwa mwenye kutawala maswala mengi ya kisiasa mjini Baghdad ) mnamo mwaka 1968 Sheikh Yaaqubiy alihamia Baghdad kumfuata baba yake.

Ameanza kuchuma elimu na maarifa ya kidini tangu akiwa na umri mdogo sana, kwani alikuwa akihudhuria vikao vya kielimu vya baba yake, ambapo alikuwa akisikiliza kwa makini na kisha kuvifanyia utafiti kwa mapana zaidi anapokuwa anarejea kwa mama yake (Mungu amrehemu).

Na hata baba yake alikuwa akichangia sana kutambulisha ujuzi na kipaji cha mtoto huyu mbele ya maulama wakubwa wa kipindi hicho. Sheikh Yaaqubiy alianza kusoma na kurejea vitabu ili hali akiwa bado chini ya miaka kumi, jambo ambalo lilipelekea kutunga kitabu kiitwacho “Alkhamru amil Khabaith” hali ya kuwa hata bado hajafikia umri wa kubalehe. Na hata vitabu ambavyo alikuwa akivisoma ni vitabu ambavyo vilikuwa vikiongezeka undani wake kila ambavyo miaka inasonga.

Ilipofikia mwanzoni mwa miaka ya sabini, Sheikh Yaaqubiy alijiunga na Shule ya masomo ya dini ambayo ilikuwa imeasisiwa na Marhum Sayyid Ally Al Alawiy katika kitongoji ya Al Abidiy mjini Baghdad.

Alishiriki na kumaliza masomo yake ya akademia  na kuchukua shahada ya kwanza ya uhandisi katika chuo cha uhandisi mjini Baghdad mnamo mwaka 1982, ambapo baada ya hapo alitakiwa kujiunga na kuhudumia jeshi kama ambavyo inatakiwa. Na kipindi hicho vita ya Iraq na Iran ilikuwa ndio imepamba moto, alishindwa kujiunga na jeshi hilo kutokana malezi ya kidini ambayo yalikuwa ni kizuizi kikubwa cha yeye kujiunga na jeshi la kupambana juu ya dhulma na kuwa moja ya wenye kueneza dhulma hata kwa muda mchache.

Hivyo alichukua uamuzi wa kujifungia ndani, japokuwa jambo hili ilikuwa ni hatari kwa maisha yake, kwa maana askari walikuwa wakikatiza kila wakati katika miji hasa Baghdad na kuwashambulia kwa risasi mbele ya hadhira  wote wenye kupinga amri ya kujiunga na jeshi katika vita.

Baada ya kukamilisha masomo yake, Sheikh Yaaqubiy akaanza rasmi kazi ya utunzi na uandishi wa vitabu, moja ya vitabu vyake ni kama “Daurul Aimma fil Hayatil Islamiya” bila ya kuwa na mwenye kumsaidia katika hilo, tena katika mazingira magumu kama yale. Mapaka pale Mwenyezi Mungu alipojaalia ikapatikana njia ya siri na yeye kuweza kuwasiliana na Sayyid Shaheed Sadr Thani, na hiyo ilikuwa ni mwaka 1985. Jambo ambalo lilipelekea kuzalisha baadhi ya vitabu na maandiko mengi mno katika uwanja wa Fikra za Kiislamu, adabu, kuilea nafsi na vinginevyo, ambayo yote haya yalitokana na kurejea kwake vitabu viwili ambavyo ni “...Ashahid Sadr Thani kama Aarifuhu” na “Qanadilul Arifina”. Ambapo pia Sayyid Sadr Thani kupitia fikra hizo aliweza kuandika tunzo kubwa mno kama vile “..Ma waraal Fiqh” na kitabu cha “..Nadhratun Fii Falsafatil Ahdaath..”.

Baada ya kumalizika kwa vita vua Iran na Iraq mnamo mwaka 1988, Shekhe alirejea mjini Najaf na kuweza kufunga ndoa na Binti wa Allamha Sayyid Muhsin Al Musawiy Alghariifiy, ambaye alikufa shahidi katika tukio maarufu la “..Intifadha Shaabaniya..”. tukio ambalo Shekh mwenyewe pia alishiriki pamoja na waandamanaji wengine wa mji wa Najaf katika harakati za kuutetea mji wa Karbala baada ya nguvu za dola kuuvamia, lakini waandamanaji walimchukua Sheikh na kumrejesha Najaf hivyo hakupata nafasi ya kushiriki katika mapambano hayo.

Lakini aliweza kutumia fursa ya uandishi kwa kuandika maelekezo muhimu sana ambayo yaliweza kuinua nguvu za vijana katika  kunusuru na kushinda tukio lile, maelezo ambayo baadhi yake yaliweza kusomwa na kukaririwa katika viunga vya Haidary ndani ya haramu tukufu.

Na baada ya kushinda wananchi katika tukio hilo, walimchangua Ayatollah Sayyid Shahid Sadr thani kuwa kiongozi wa mapinduzi hayo, ambaye naye baada ya siku moja alijiuzulu cheo hicho huku akiwa ameacha tayari vitengo vitano katika kuendesha mapinduzi, ambapo Sheikh Yaaqubiy alikuwa mkuu wa kitengo cha siasa na habari.

Hata hivyo vitengo hivyo havikuweza kutekeleza majukumu yake, kutokana na nguvu za dola ya Saddam  kushambulia  mji wa Najaf siku ya pili tu tangu kuasisiwa kwake.

Mnamo mwaka 1992 sawia na mwezi Shabani mwaka 1412, Shekhe Yaaqubi aliweza kuvaa vazi maalumu la ulama wa dini kwa mkono wa Ayatollah Udhma Sayyid Khui (qs).

Pia Sheikh Yaaqubiy ni katika watu ambao walikuwa tegemeo la kwanza la Sayyid Shahid Thani katika harakati za mwanzo kabisa za kutangaza Marjiiya yake mwanzoni kabisa mwa mwaka huo, na haya yamenukuliwa kutoka kwa Sayyid Shahid Sadr mwenyewe katika baadhi ya mahojiano yake yaliyokuwa yakisajiliwa. Hii ilikuwa i pamoja na Shekhe Yaaqubiy kuwaridhisha waliokuwa naye katika hauza na mashule katika swala zima la kurejea kihukumu kwa Sayid Shahid Sadr (qs). Jambo ambalo lilipelekea kutanuka na kujulikana kwa Sayyid Sadr na kisha Sheikh Yaaqubiy mwenyewe kuwa ni mtu wa pili baada ya Sayyid Sadr kuchukua nafasi hii ya Umarjii.

Aidha Sayyid Shahid Sadr alimfanya Sheikh Yaaqubiy kuwa ndio nguzo na mkuu wa chuo cha Sadr baada tu ya kuasisiwa, chuo ambacho kilianzishwa kwa makusudi ya kuweza kuoanisha na kukutanisha baina ya elimu za vyuo vya kidini na vyuo vya akademia. Ambapo Sayyid Sadr hakuona mwenye uwezo wa kufikia katika malengo haya zaidi ya Sheikh Muhammad Yaaqubiy, na hii ni kutokana na kwamba yeye alikuwa ameshavuka ngazi nyingi katika nyanja zote mbili, kama ambavyo Sayyid aliweka wazi siku ambayo alikuwa akimkabidhi majukumu hayo mwezi wa Safar mwaka 1419.

Mbali na hapo pia Sayyid alikuwa akiashiria kunako nukta hii katika sehemu mbalimbali, kama vile katika utangulizi wa kitabu cha “Almushtaqu indal Usuliyin”  na pia katika “Qanadilul Arifin”, na hata miezi mitano kabla ya kufariki kwake Sayyid aliashiria kwamba Sheikh Yaaqubiy ndio atakuwa mrithi wake, ilikuwa ni tarehe 5 Jamadul Thani mwaka 1419 sawa na tarehe 29 mwezi wa 9 mwaka 1998, ambapo ilikuwa ni katika mkutano wake na wanafunzi wa chuo kikuu cha Sadr. Ambapo alinukuliwa akisema:

“...Naweza kusema kwamba Sheikh Muhammad Yaaqubiy  ndiye mtu pekee ambaye anaweza kuwa chaguo katika kusimamia chuo baada ya pale ambapo Mwenyezi Mungu atanijaalia umri, na nashuhudia juu ya uwezo wake, kwa hiyo yeye ndio anatakiwa kushikilia Chuo hichi baada yangu....”.

Hivyo Sheikh Yaaqubiy akarithi uongozi wa hauza kwa mujibu wa misingi yake, ambapo moja kwa moja akaanza kueneza baadhi ya bahthi zake katika nyanja za kidalili ambazo alikuwa ameziandika tangu mwaka 1420, jambo ambalo lilipelekea mwaka 1424 sawa na mwaka 2004 Ayatollah Sheikh Muhammad Ally Al Karami kushuhudia uwezo wake katika kutoa dalili za kisheria (Ijtihad). Ambaye naye aliweza kupata Ijaza (Ruhusa) ya Ijtihad kutoka kwa Ayatollah Sheikh Muntadhariy, ayatollah Sheikh Muhammad Sadiq Tehraniy, Ayatollah Sayyid Al Khui mwaka 1386 na wengineo, Inshallah Mwenyezi Mungu awahifadhi waliopo na awarehemu waliotangulia.

Sheikh Yaaqubi alikuwa sambamba sana na Sayyid Shahid Sadr mpaka wakati wa mauti yake, na yeye ndio alisimamia sala yake pamoja na ibada ya kumsitiri katika nyumba yake ya milele akishirikiana na baadhi ya wengine wachache katika mazingira yale yaliyokuwa ni yenye kutisha kipindi kile, mazingira ya watawala wenye kutumia mabavu na nguvu pamoja na silaha.

Aidha Sheikh Yaaqubiy aliweza kusimamia na kuendeleza harakati ya Kiislamu ambayo ilianzishwa na Sayyid Sadr nchini Iraq, hii ni pamoja na kuanzisha nyenzo nyingine kabisa baada ya kuwa zile zilizokuwa zimeanzishwa na Sayyid Sadr kuzimwa na dola, na miongoni mwa nyenzo hizo ni pamoja na sala ya Ijumaa.

 

Elimu yake ya Dini

Pamoja na kuwa ni mwenye elimu ya maswala ya kijamii, pia Sheikh Yaaqubiy alianza kuchukua elimu yake ya dini kwa ngazi ya kati (masomo kama vile Al Lumua na Usulul Fiqh) katika chuo cha dini mjini Najaf chini ya uangalizi wa Al Marhum Sayyid Muhammad Kalantar (qs), ambapo aliweza kuvuka na kufaulu kwa ngazi za juu kutokana na juhudi yake. Baada ya kuingia katika ngazi za juu muda huo huo kwa ushauri wa Sayyid Shahid Sadr aliweza kujiunga pia na masomo ya juu kabisa (Bahthul Kharij), ambapo alikuwa akihudhuria masomo ya Usulu Lafdhiyah kwa Sayyid Sadr mwenyewe kuanzia Shawwal 1414 Hijiria mpaka siku ambayo Sayyid aliaga dunia. Aidha pia alihudhuria masomo ya Usulul Amalia  kwa Ustadh Ayatollah Sheikh Muhammad Ishaq Al Fayadh kuanzia mwaka 1417 mpaka mwaka 1421.

Na upande wa Fiqh aliweza kuhudhuria darasa za Ayatollah Sayyid Sistani kuanzia mwaka 1415 mpaka mwaka 1420. Pia kwa Marhum Shahid Mirza Ally Al Gharwiy kuanzia mwaka 1416 mpaka 1418, pamoja na kuandika Taqriri zote za masomo yake.

Sheikh Yaaqubi alianza kwanza kufundisha masomo ya msingi katika dini kabla ya mwaka mmoja mbele kujiunga na Hauza ya Kielimu katika mji wa Najaf, ambapo taratibu alianza kufundisha ngazi ya kati katika masomo ya Al Lumua na Usulul Fiqh, na pia ngazi ya juu katika masomo ya Makasib na Al Kifaya. Na inasimuliwa kwamba darasa lake ndilo lilikuwa darasa lenye wahudhuriaji wengi na lenye kunufaisha zaidi ya mengine.

Mnamo mwaka 1427 Sheikh Yaaqubiy alianza kutoa mihadhara yake ya Fiqhi kwa ngazi ya elimu ya juu kabisa (Bahthul Kharij), ambapo alichagua maudhui ya mambo yenye kutofautiana baina ya madhehebu kuwa ndio maudhui kuu ya mihadhara yake hiyo. Ambapo katika hilo alikuwa akichagua mambo ya kielimu ambayo ni ya kina na mijadla baina ya maulama ili elimu iweze kuchukua nafasi yake zaidi. Ambapo kwa sasa zaidi ya walimu wapatao 200 kutoka katika vyuo vya dini mbalimbali wanahudhuria somo lake hilo.

Na mpaka sasa tayari ameshanakili masiala mengi ya muhimu katika nyanja za kielimu, na baadhi ya hayo tayari yameshachapwa katika kitabu chake cha “Fiqhul Khilaf” ambacho mpaka sasa juzuu kumi tayari zimeshatoka. Juzuu ambazo zimekusanya masiala 51. Na moja ya jambo la pekee katika mihadhara yake ni pamoja na kutumia sana rai na mitazamo ya maulama wa zamani pamoja na wa sasa wa vyuo vikubwa vya Najaf pamoja na Qom.

Tayari ana Risala yenye jina la “Subulul Salam”, ambapo tayari Juzuu ya kwanza imeshatoka tangu mwaka 1430, kama ambavyo pia ana risala yenye kuzungumzia matendo ya Hijja ambayo imerudiwa kuchapwa mara kadhaa.

 

Vitabu vyake

1.   Fiqhul Khilaf:

Ambacho tayari juzuu tisa zimeshatoka. Kitabu ambacho anaweka ndani yake mihadhara yake ambayo alikuwa akiitoa katika masomo yake ya juu (Bahthul Kharij) katika mji mtukufu wa Najaf.

2.   Alfiqhul Bahir Fi Swaumil Musafir (Fiqhul Istidlal Muamiq).

3.   Khitwabul Marhala.

Ambacho mpaka sasa kuna juzuu tisa ambazo zimeshatoka. Katika kitabu hichi kinakusanya baadhi ya hotuba zake ambazo alikuwa akizitoa tangu mwanzoni kabisa mwa kupokea majukumu ya kusimamia harakati ya Kiislamu nchini Iraq, na hii ilikuwa baada ya kufariki shahidi Sayyidi Sadr Thani mwaka 1999. Na katika hotuba hizo amejaribu kuzipanga kwa mujibu wa tarehe ambazo zinakusanya matukio muhimu katika historia ya Iraq na harakati ya Kiislamu kiujumla.

4.   Al Uswatul Hasanah lilqaadatil wa Muslihina.

Kitabu cha juzuu moja ambapo ndani yake anazungumzia maisha ya Mtume Muhammad (saww) kwa uchunguzi wa kina, ikiwa ni pamoja na kuashiria mafunzo na mazingatio yanayopatikana humo.

5.   Daurul Aimma fil Hayatil Islamiyah.

Kitabu cha juzuu moja pia chenye mfumo wa kitabu kilichopita, ambacho hichi kinazungumzia maisha ya Maasumina as pamoja na malengo shirikishi ambayo kwa pamoja walifanya juhudi katika kuyafikia. Pia katika kitabu hiki kuna baadhi ya nukta alizoashiria Ayatollah Sayyid Al Khui ra.

 

6.   Al Maalimul Mustaqbilah Lil hauzatil Ilmiyah. Juzuu moja.

7.   Alriyadhiyati lil faqiih. Juzuu moja.

Kitabu cha kipekee sana ambacho ndani yake anasherehesha baadhi ya misingi ya kihesabu kwa ajili ya milango mbalimbali ya Fiqhi.

8.   Al Mushtaqu Indal Usuliyin. Kitabu cha juzuu mbili.

Ambapo ndani yake kuna ripoti na takriri zake juu ya mihadhara ya Sayyid Shahid Sadr ra katika nyanja za elimu ya Usulu katika mada ya “Al Mushtaq”.

Sayyid alichapa kitabu hichi pamoja na vitabu vyake vya Usulu “Minhajul Usul..”

9.   Al Shahid Sadr Thani kama Aarifuhu.

Kitabu cha juzuu moja ambacho ndani yake an=mekusanya mihadhara ya Sayyid Shahid Sadr, pamoja na barua au bahthi ambazo walikuwa wakizifanya kwa pamoja.

10.  Qanadilul Arifin.

Kitabu cha juzuu moja ambacho kinakusanya baadhi ya barua ambazo walikuwa wakitumiana baina yake na Sayyid Shahid Sadr hasa katika nyanja za kuilea nafsi pamoja na njia za kuweza kumfikisha mja kwa Mwenyezi Mungu. Barua ambazo zinarejea miaka ya 1987.

11.  Thalathatun Yashkun

Kitabu ambacho kinakusanya juzuu tatu zenye kuelezea vitu vitatu vyenye kushitakiwa kwa Mwenyezi Mungu swt. Quran, Msikiti na Imamu (as). Na tayari vyote hivi vimeshachapwa.

 

12.  Al Fiqhul Ijtimaii.

Kitabu cha Juzuu Tatu ambacho kinakusanya fatwa za kijamii kutoka kwake mwenyewe chini ya mtazamo wake ambao unajulikana kama “Al Ususul Aamma Lil Fiqhil Ijtimai”.

 

13.  Nahnul Wal Gharbi.

Kitabu ambacho kinaelezea baadhi ya misingi ya tamaduni za Kimagharibi ikiwa ni pamoja na kubainisha ubora wa misingi ya tamaduni za Kiislamu.

 

14.  Min wahyil Ghadeer

15.  Fiqhu Twalabatil Jamiati

Ni vingine vingi.

Ukizingatia upana wa uhitajiwa jamii hasa maswala ya vitabu, Shekhe Yaaqubiy alikuwa pia akiwapa baadhi ya wanafunzi wake bora majukumu ya kuhariri na hata kutunga baadhi ya vitabu pia.

Kwa maana Shekhe alikuwa akitoa fikra mama juu ya kitabu husika, pamoja na kuwasimamia katika uandishi wao ili tu waweze kufikia katika kukidhi haja kutokana na uhitaji wa watu katika sekta hiyo. Na hii ni baada ya kuhisi kwamba ili kuvuka vikwazo na changamoto zilizopo haitakuwa rahisi yeye peke yake kufanikisha. Pia ni katika njia ya kueneza uwezo kwa wengine, ambapo tunakuta kwa njia hii idadi ya vitabu vingi mno viliandikwa, na vyote vilikuwa ni katika kuziba yale mapengo au haja ya jamii kwa mujibu wa fikra zake Shekhe.

Aidha pia mamia ya mihadhara juu ya tabia, fikra na jamii katika nyanja tofauti ilisajiliwa.

 

Miradi yake

Ayatollah Yaqubiy anaamini kwamba kazi zozote zile za Marjii haziwezi kuendeshwa na watu kadhaa, bali ni lazima kuwepo na taasisi. Hasa hasa baada ya kutanuka kwa majukumu baada ya kuisha na kuanguka utawala wa Saddam mnamo mwaka 2003. Na hapo ndipo Sheikh alipopata nafasi ya kuweza kuingia katika sekta ambazo zilikuwa si rahisi kabla ya hapo, kama vile sekta za media.

Na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mnamo mwaka 2003 huo sawa na 27 Safar 1424 Hijiria, aliweza kuweka mkutano wa kuasisi taasisi ya “Jamaatul Fudhalaa”.

Taasisi ambayo inakusanya watu kutokea katika vyuo vya kidini, watu  wenye mchangamko na harakati mbalimbali za kijamii pamoja na mwamko wa harakati za Kiislamu zenye nia ya kuuzindua umma. Ambapo watu hawa wanakuwa na majukumu ya kuongoza zile nukta kutanishi baina ya taasisi zenye kuwahusu.

Na watu ambao walikuwa mstari wa mbele kabisa katika harakati hii ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Sadr, ambao walichukua mafunzo ya kielimu, adabu na fikra kutoka kwake Shekhe mwenyewe.

Kama ambavyo pia Sheikh aliweza  kutembelea mji wa Najaf na kubakia takriban siku tatu. Ambapo alipata nafasi ya kuongoza sala ya Ijumaa iliyofanyika katika ukumbi wa Kadhimi mnamo tarehe 22 Safar sawa na 25/4/2003. Ambapo aliweza kutumia nafasi hiyo kuwaelekeza maelfu ya watu waliohudhuria kunako mambo wanayotakiwa kushikamana nayo katika kipindi kile cha mageuzi. Pia alitumia muda huo kuwaalika wote kuhudhuria katika maandamano ya amani yaliyofanyika  katikati ya mji wa Baghdad katika siku iliyofuatia, maandamano yenye lengo la kutilia mkazo azma ile. Maandamano ambayo yalishuhudia umati mkubwa sana wa watu wakijaza mitaa.

Pia katika ziara yake hiyo aliweza kukutana na baadhi ya walimu wa shule za akademia pamoja wanaharakati wengine wa kijamii, ambapo Sheikh kwa mara nyingine alitumia nafasi hiyo kuwasihi na kuwashauri wafuasi wake kunako umuhimu wa kutengeneza vikundi vya Kisiasa na kushiriki katika siasa hasa baada ya kuanguka kwa utawala wa Saddam, hii yote ili tu kuweza kupata nafasi ya kutekeleza malengo ya Kiislamu na hata nchi pia kwa mujibu wa ule mpango wa kikundi cha “Alfadhilat Islamiya”.

Ambapo mpango huu kwa kiwango kikubwa uliweza kufanikiwa, na kuweza kupata wawakilishi wengi katika Bunge la nchi.

Kama ambavyo pia Sheikh aliweza kutoa nasaha zake kwa watu mbalimbali kama vile walimu wa vyuo, wahitimu wa masomo, wahandisi wa Kiislamu, kina mama na wengineo, kunako umuhimu wa kucheza katika nafasi zao huku akitoa ahadi za kusimamia harakati hizo.

 

Zifuatazo ni baadhi ya taasisi ambazo mpaka sasa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu zimeweza kusimama, ukiachilia mbali ile ya “Jamaatul Fudhalaa”.:

1.   Chuo kikuu c ha kidini Cha Sadr.

Chuo ambacho kilianzishwa mnamo mwaka 1417 sawa na mwaka 1997 chini ya usimamizi wa Yatollah Sayyid Shahid Sadr (ra).

Lengo kuu hasa la kuasisiwa kwa chuo hiki ilikuwa ni kuwavuta wanafunzi na wahitimu wenye shahada za Kiakademia, kuja upande wa elimu za dini, na kisha kuwakusanya katika mradi wenye lengo la kukusanya baina ya elimu hizi mbili.

Sasa baada ya kuasisiwa na Shahid Sadr Awwal, kishakuja kuendelezwa na Shahid Sadr Thani, pia Sheikh Yaaqubiy akaja kuweka nguvu zake hapo kutokana na kwamba yeye Mwenyewe ni kuhitimu wa masomo ya akademia kwa daraja za juu sana, kama ambavyo pia upande wa elimu za dini pia ilikuwa hivyo.

Sheikh alitumia hekima na ushijaa mkubwa mno katika kuhifadhi na kuendeleza chuo hiki, hasa baada ya kufariki Muasisi wake na kuanguka kwa utawala wa Saddam, ambapo aliweza kufungua matawi kadha wa kadha katika miji mbalimbali, ambapo mpaka sasa kuna zaidi ya matawo 20 na zaidi ya wanafunzi 2000 ndani yake.

Ambapo katika hayo matawi sita yapo katika mji wa Baghdad na manne yapo mjini Najaf hii ikikusanya na chuo mama.

Sheikh aliweza kuandaa misingi ya vyuo hivi vyote ikiwa ni pamoja na nidhamu zake na namna ya utendaji kazi wake katika kitabu kimoja alichokipa jina la “..Jamiattul Sadr Diiniya, Al Huwiya wal Injazat..”

Muda wa masomo katika vuo hivi ni miaka nane, ambapo miaka mitatu ya mwanzo kunakuwa ni ngazi ya maelekezo ya kidini na kujenga jamii, miaka mitatu ya pili inakuwa ni kwa ajili ya kuwaandaa walimu na wakufunzi, na inayobakia inakuwa ni kwa ajili ya ngazo ya juu kabisa ambayo i “Ijtihadi”.

Kuna idadi kubwa mno ya wahitimu mpaka sasa kutokea katika vyuo hivi.

 

2.   Jamiatul Zahra (as) Lil Ulumi Diniya.

Na chuo hiki pia kipo katika misingi ya chuo cha Sadr, hasa katika upande wa misingi na nidhamu zake. Isipokuwa tu chuo hiki kiliasisiwa baada ya kuanguka kwa utawala wa Saddam mwaka 2003, ikiwa i maalumu kwa kina mama.

Mpaka sasa chuo hiki kina matawi yapatayo 14 katika mji wa Najaf na miji mingineyo kiiwa kinakusanya mamia ya wanafunzi.

Chuo hiki kinalinda sana katika mafunzo yake, majukumu ya mwanamke katika jamii na kazi zake, ambapo katika chuo hiki pia kuna tawi maalumu kwa ajili ya kuwaandaa kina mama wenye uwezo wa kuhutubia katika mimbari mbalimbali.

 

3.   Rabitatul Banatil Mustafa.

Taasisi maalumu kabisa kwa ajili ya kupangilia majukumu ya kijamii ya mwanamke.

Ambapo tawi kuu lipo Baghdad na matawi mengine yakiwa katikamiko mingine. Vyuo hivi vinasimamia kwa ukaribu zaidi baadhi ya harakati mbalimbali za kijamii kupitia taasisi nyingine, kama vile kulea wajane na watoto, kuwaandaa kina mama na kuwapa elimu za Fiqh na itikadi, kusaidia wasiojiweza, kuandaa masomo maalumu katika nyanja za kina mama, mafunzo ya matendo kama vile kompyuta, ushonaji, huduma za kwanza za afya, kusimamisha baadhi ya mambo ya kidini na matukio ya kijamii kwa pamoja, kujaribu kusimamia maswala ya ndoa na mengineyo. Ambapo Sheikh mwenyewe ameandaa waraka maalumu katika kuelezea kazi na misingi ya vyuo hivi vyenye kubeba aina ya kina mama ambao wana uwezo wa kufikisha ujumbe wa Kiislamu katika nyanja mbalimbali za kijamii na hata Kisiasa pia.

 

4.   Kikundi cha “..Alfadhilatul Islamii..”

Miongoni mwa harakati za Shekhe i pamoja na kuanzisha kikundi cha kisiasa ambacho kitakuw ana ushiriki katika upande wa siasa baada tu ya kuanguka kwa utawala wa Saddam mwaka 2003.

Hii ni kwa ajili ya kuweza kufanikisha na kutimiza malengo ya nchi na dini kwa pamoja kupitia kikundi hiki kwa jina la “..Alfadhilatul Islamiyah..”.

Katika kikundi hiki aliweza kuchagua baadhi ya watu wenye elimu za akademia na kuwaingiza katika upande wa siasa, na mpaka sasa tayari ana wawakilishi wake katika ngazi ya serikali za vijiji mpaka Bunge la nchi.

Ratiba na mikakati yake kisiasa ina tofautiana sana  na mikakati na ratiba nyinginezo, kwani ratiba yake imejikita zaidi katika mambo ya kutetea nchi, Dini, Utu pamoja na kuweka kando mambo yote ya kujiona na kujitenga, au kutawanya watu kwa makundi makundi.

Na amejaribu kuandika baadhi ya misingi na mikakati yake ya kinidhamu katika kitabu alichokipa jina la “.AL Usuu Nadharia lihizbil fadhilatil Islamiya..” au “Al amalu Siyasi minal wajibiati Shar Iya” au “..AL Mabadiu Thabitah fi Siyasah..” au “Mabadiul Shafiyah wa anasiriha fi Madrasatil Ahli Bayt (as)”.

Pia ameweza kuandika mipango yake ya kisiasa pamoja na sifa mahususi za kikundi chake hicho, kama ambavyo pia ameandika kunko nidhamu yenye kuifaa nchi ya Iraq au kitabu kwa jina la “..Limadhal Fadhilatu Hizba?”.

Pia Sheikh ameweza kubainisha uhusiano uliopo baina ya Jamaatul Fadhila na Hizbul fadhila katika nyanja kuu nane.

Kikundi hichi  ni mkusanyiko wa uongozi mkuu wambao upo mjini Baghdad, ambapo chini yake hapo kuna vitengo vya siasa, habari na uenezi, utendaji, mikakati na mipango, kuendeleza vipaji katika nyanja tofauti na mengineyo. Kama ambavyo pia kuna matawi katika mikoa mingine.

5.   Niqabatul Sadatil Alawiyina.

Ambapo lengo la kuasisiwa kwake ni kuweza kutukuza na kutambua utukufu wa kizazi cha mtukufu Mtume Muhammad saww kupitia watoto wa bi Fatima zahraa as.

Ikiwa ni pamoja na kukidhi haja zao na kuozesha vijana wao. Taasisi hii ina makao makuu mjini Najaf na matawi sehemu nyinginezo. Pia taasisi hii ina wawakilishi wake Bungeni chini ya mpango wa  kile kikundi cha Fadhilatul Islamiya.

Sheikh ameandika mengi sana katika kuelezea sababu na malengo ya kuasisiwa kwa kikundi hiki, ikiwa ni pamoja na kuelezea mikakati na namna ya utendaji kazi wake.

6.   Kikundi cha Wahandisi wa Kiislamu.

Ambapo ni sehemu kubwa ya nguvu za kiuchumi na kifani katika taasisi nzima ya kueneza ujumbe.

Na hii ni kutokana na kwamba Iraq ina idadi ya Wahandisi wapatao laki moja, ambapo ndani yake idadi kubwa mno ni waumini na wenye kuamini juu ya ujumbe wa dini. Hasa ukizingatia kwamba nchi ipo katika kazi ya kujenga jamii mpya yenye kushikamana na dini, hivyo kuwakusanya watu kama hawa na kuwapa nafasi katika kujenga Iraq mpya kutaweza kusogeza kwa kiasi kikubwa nafasi ya kufikia malengo.

Na mpaka sasa mashirika ambayo yapo chini ya vikundi hivi yameweza kufanya kazi katika nyanja ambazo si nyingi kama ambavyo inahitajika, na hii ni kutokana na kukosekana kwa nyenzo ambazo mpaka sasa kwa hazijatimia, na Mungu akitaka zitatimia kwa uwezo na mapenzi yake.

7.   Wanazuoni

Taasisi ambayo inakusanya walimu, wanafunzi, watendaji wa idara wa vyuo mbalimbali nchini Iraq.

Sheikh ameandika kitabu maalumu kabisa kwa jina la “Kiyanu Jamiiyuun, Al Ahdafu wal Amal”  ambapo ndani yake ameeleza kwamba kuasisiwa kwa kikundi hiki ni katika kufanyia kazi wito wenye kuelekezea watu kunako umoja kupitia vyuo. Ambapo mpaka sasa ina

kadiriwa kuwa ni taasisi pekee ambayo haijafikiwa na fitina za kikabila au kisiasa. Ukiachilia mbali kuitika wito huu bado taasisi hii ina malengo mengine makubwa kama vile kutilia umuhimu harakati na maswala ambayo yanasimamiwa na vyuo katika uwanja wa kuendeleza na kukuza nchi kwa ujumla.

Taasisi hii ilianzishwa mnamo mwaka 2006, na Shekhe aliweza kuwahutubia katika mkutano wao wa kila mwaka uliofanyika mjini Karbala katika masiku ya Ashura mwaka 1428. Mkutano ambao umeanzishwa kwa lengo kuhuisha maeneo ya elimu na dini.

8.   Kikundi chenye kusimamia mikakati na nidhamu ya miji.

Ambapo inakusanya sehemu mbalimbali za kidini katika utendaji wake.

Makao makuu ya taasisi na kikundi hiki yapo Baghdad na matawi yake mengine yapo katika miji tofauti.

Baadhi ya sekta za kikundi hiki zi zenye kuhusika na maswala ya kijamii na nyinginezo ni katika sekta za tiba na kusaidia wengine. Na kuna wengi sana ambao hujitolea kufanya kazi katika taasisi hizi bila malipo, hasa vijana ambao wana roho ya dini.

Na Sheikh ana mazungumzo mengi sana katika kuzungumzia umuhimu wa taasisi hizi, ikiwa i pamoja na kuzitanua na kuandaa mazingira ya utendaji kazi wake.

 

 

9.   Taasisi za habari na media.

a.     Chaneli ya Al Naim.

Ambapo ni chaneli ya kidini yenye nia ya kukuza na kueneza mafunzo ya Ahlu Bayt katika sekta za jamii, adabu na nyinginezo.

Na imeweza kukidhi haja kubwa sana ndani ya Iraq. Inarusha matangazo yake kutokea mjini Basra lakini ofisi yake kuu ikiwa mjini Najaf na Baghdad, na huku ikiwa na matawi katika miji mingine.

Sheikh katika uwanja huu pia ana maneno kuhusu umuhimu wa media pamoja na mchango wa maneno na mazungumzo katika maisha ya kibinadamu.

b.    Idhaa ya Al Bila mjini Baghdad

c.     Idhaa ya Al Amal mjini Basra

d.    Idhaa ya Subul Sala mjini Nasiriyah

e.     Idhaa ya Al Ramitha katika mkoa wa Al Samawah.

Pia katika moja ya harakati zake ni pamoja na kuasisi usomaji wa ziara ya Bi Fatima katika kaburi la Imamu Ally as siku ya 3 jumadul Thani kila mwaka, katika kuadhimisha siku ya kufariki dunia bi Fatima Zahra (as).

Ambapo ni katika harakati zenye kuchangia kwa kiasi kikubwa mno ufikishaji wa kadhia ya kifo cha Bi fatima Zahra (as), pamoja  na kuonyesha athari zake kubwa.

Maelfu ya waumini hushiriki katika kusindikiza mfano wa jeneza la Bi Fatima kuelekea katika kaburi la Imamu Ally (as) kisha Sheikh hutoa hotuba. Na harakati hii ilianza rasmi kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1427 sawa na mwaka 2006.

Kama ambavyo pia baada tu ya kuanguka kwa utawala haramu wa Saddam, Sheikh aliweza kuanzisha Mawakib (Vituo vyenye kutoa huduma kwa ajili ya Imamu Hussein as) vya walimu na wanafunzi wa vyuo, ambapo zaidi ya watu elfu 20 hushiriki katika huduma hizo kila mwaka ndani ya Karbala katika kuadhimisha tukio la ashura na kifo cha Imamu Hussein (as).

 

Misingi muhimu ya harakati za kiongozi wa Dini

Harakati ya Ayatollah Sheikh Mihammad Yaaqubiy imejengeka katika misingi na taratibu mbalimbali, lakini katika vitabu na hotuba zake amekuwa akigusia na kutilia sana mkazo baadhi yake, ambazo ni:

1.   Kuwa na nia thabiti na Mwenyezi Mungu swt (Ikhlas).

Kwa maana ya kwamba ridhaa na kuridhiwa na Mungu iwe ndio lengo kuu katika harakati. Hivyo mipango, malengo vyote viwe kwa mujibu wa Mwenyezi Mungu (swt).

 

2.   Kutaraji kuwa karibu na Mtume, Maimamu pamoja na kutegemea Quran na Sunna kama njia za kurejea katika kutoa hukumu, na pia kufanya ndio desturi na msingi wa uongozi.

3.   Kumkrimu mwanadamu.

Kwa maana ya kwamba kumfanya kuwa ni lengo la juu kabisa, na kila kitu ambacho utakuwa unakifanya basi kiwe ni katika kuhakikisha usalama wa maisha yake.

 

4.   Umoja na muungano.

Kwa maana ya kuwa na utofauti katika kutekeleza majukumu, na uweka kando migongano na kila lenye kupelekea kutofautiana na kutengana.

 

 

5.   Umakini katika uchagua viongozi wa Umma.

Na hii ni kwa mujibu wa vigezo sahihi, kwa maana kuongoza umma kwa njia sahihi ndio jambo ambalo kwalo umma utaweza kutengemaa.

6.   Kuilea nafsi katika misingi na adabu njema, na kutakasa nyoyo zetu kwa kiwango ambacho zitamjia Mwenyezi Mungu zikiwa safi.

7.   Kuuokoa Umma kutoka katika ujinga na kutofautiana na kudhaniana vibaya, ikiwa ni kwa kutengeneza hali ya watu kujitambua na kushikamana na dini na uchamungu.

8.   Kuutngaza Uislamu sahihi.

Kwa kuonyesha nguvu na nukta za nguvu zake, na kuweza kuwakinaisha watu katika kujiunga nao na kuufuata. Pamoja pia na kuashiria kunako mapungufu ya nidhamu za kimaada (zisizofuata misingi ya Dini). Kama ambavyo pia kuonyesha namna ambavyo elimu na nadharia peke yake zilivyoshindwa kuleta ukamilifu katika maisha ya watu.

 

9.   Nidhamu na umakini katika utendaji wa taasisi kiasi kwamba wote watavutika.

10.                    Kupambana na ufisadi na uhalifu.

Pamoja a dhulma, kujiona, kutawala kwa mabavu bila haki, pia kulingania watu kunako kusaidia wasiojiweza kwa kila hali.

 

 

 

Baadhi ya maneno ya Shahid Sayyid Sadr Thani kuhusu Sheikh Mohammad Yaaqubiy ra.

 

1.   Katika Utangulizi wa kitabu chake cha AL Mustaq, Sayyeid Shahid Sadr amenukuliwa akisema:

“...Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma na mwenye kurehemu.

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu na sala na salamu ziende kwa Mtume Muhammad saww pamoja na kizazi chake.

Laana zenye kudumu pia ziwe juu ya maadui zao wote.

Ama baada, hakika katika neema za Mwenyezi Mungu kwa dini na madhehebu kwa ujumla na hasa kwangu mimi nikiwa kama mja mwenye madhambi na makosa, ni kuniruzuku idadi ya wanafunzi wenye nia safi, juhudi, ambao huwezi kuwaweka daraja ya chini kamwe, Mwenyezi Mungu awalipe heri na malipo ya walio wema. Na miongoni mwao ni huyu Sheikh Mtukufu, mwenye elimu kubwa, Sheikh Muhammad Yaaqubiy. Kwa maana ameshiriki masomo yetu ya Usul na kuyapa kipaumbele mno katika kuyafahamu na kuyaandika pia. Na ndiye huyu ambaye katika kitabu hiki anajaribu kutuonyesha baadhi ya juhudi zake na upevu wa fikra zake, nami nimejaribu kukirejea na kukitilia maanani, nikakuta kwmaba ni chenye kujitosheleza katika kutimiza malengo na chenye kukusanya mambo yote ya Elimu ya Usulu. Na mimi natambua kuwa yeye ndio kama mtunzi wa kitabu hiki, na hata yeye mwenyewe ana haki ya kujitambua hivyo japokuwa kitabu na maswala yake yote ni kutoka kwangu, ila natoa ruhusa hii kwa sharti la kuhifadhi maana na madhumuni ya kitabu. Na naamini kwa juhudui zake hizi atakuwa i mwenye kupita katika njia za kufikia Ijtihadi na maarifa ya juu kabisa. Namuombea mustakabali wenye mwanga katika kutumika elimu na kuifanyia kazi, na we ni katika marajii wenye nia ya kweli na viongozi wema. Mwenyezi Mungu amlipe malipo ya watu wema, na mwisho wa maombi yetu na kumshukuru Mwenyezi Mungu mola wa walimwengu...”

Tarehe 9 Ramadhani mwaka 1418

2.   Maneno yake katika utangulizi wa sehemu ya pili ya kitabu cha Al Mushtaq anasema:

 

“..kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu.

Baada ya sala na salamu na kushukuru, kisha kuwaombea ufaulu na umri mrefu, kwa mujibu wa ufahamu wangu huu naimba niwasomee aya hii isemeyo:

“...Na uwe na subira na kwa hakika subira yako haitakuwa ila ni kwa Mwenyezi Mungu, na wala usihuzunike wala kuwa katika dhiki kutokana na vitimbi vyao, kwa hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamungu na ambao ni wema...”

Pia kwa mujibu wa ufahamu wangu i kwamba hizi takriri ambazo mmeziandika ni zenye kujitosheleza, japokuwa kwamba naweza kuongeza mambo mengine juu yake, lakini imejitosheleza na nina imani na nataraji iwe ni mwongozo wa chuo na jamii kwa ujumla.

Hasa ukizingatia kwamba ni takriri yenye kukusanya baina ya ya zamani na ya sasa, kama ambavyo mwanachuoni pamoja na mwanajamii waote wanaweza kunufaika nayo. Na kwa kweli ni jambo ambalo linastahiki juhudi zako hizi. Namuomba Mola adumishe juhudi zako na azifikishe  katika natija stahiki katika kunufaisha watu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Kwa hali yeyote ile ni jambo ambalo linahitajia sifa na pongezi pamoja na kujitolea kukubwa. Na kwa minajili hiyo naona kabisa kuna umuhimu wa kuendeleza jambo hili, na wala sioni mkabala wake kama kuna jambo ambalo linaweza kuwa sababu ya kuachana na hili, lakini maamuzi ni yako mwanzoni na hata mwishoni. Mwenyezi Mungu akulipe malipo ya watu wema na sifa zote njema ni zake....”

 

3.   Utangulizi wake katika kitabu cha Qanadilul Arifin, amenukuliwa akisema:

“...Bismillah Rahmani Rahim, Shekh mtukufu Mwenyezi Mungu adumishe utukufu wenu, naomba mtilie maanani baadhi ya nukta zifuatazo:

Najua unajua fika kuwa nilikuwa na bado nakuchukulia ni mwanafunzi wangu bora kabisa, mwenye moyo safi, muadilifu, kwa kiasi kwamba kama hapo baadaye itatokea mzozo baina ya nani anafaa kuwa Marjii basi sitakuacha, ili tu jambo hili libakie katika mikono salama, weye kukidhi haja na matakwa ya wengine, na si katika mikono ya wenye nyoyo ngumu na wenye kutafuta dunia. Na nafikiria katika mipango yangu niweze kukufanya Imamu wa sala baada yangu ili tu iwe ni maandalizi ya hilo, na bado nawaza hivyo kila siku. Na kwa kweli katika wanafunzi wangu, sijaona mwenye pande mbalimbali za kimaarifa na ambazo nimekuwa nikizitarajia kwao kama ambavyo nimeona kwako. Namuomba Mwenyezi Mungu atimize matarajio yangu kuhusu wewe kwa uwezo na msaada wake......”

1 jumadul Thani 1418

4.   Na baadhi ya maneno yake ni pale alipo hutubia chuo cha Sadr tarehe 5 jumadul thani mwaka 1419 (Kabla ya kufariki kwake kwa miezi mitano). Alisema:

“....Na sasa naweza kusema kwamba mwenye nafasi pekee katika chuo chetu ni Sheikh Muhammad Yaaqubiy, ikiwa tu Mwenyezi Mungu ataniweka hai mpaka pale nitakaposhuhudia Ijtihadi yake, kwa maana mimi sina shaka kwamba yeye ndiye anastahiki kushikilia chuo baada yangu....”.

Kwa ajili ya kutambua kwa urefu maisha ya Sheikh Yaaqubiy unaweza kurejea baadhi ya vitabu vyake alivyoandika kama vile:

1.   Shahidu Thani kama Aarifuhu

2.   Qanadilul Arifin

3.   Sheikh Mussa Al Yaaqubiy, Hayatuhu..

4.   Khitwabul Marhala

5.   Al maalimul Mustaqbaliya lilhauzatil Ilmiya.

 

 

 

 

 

 

 

 

Kutawala na kusimamia mambo ya Umma

Anuani na jambo hili linakusanya majukumu mengi mno, miongoni mwake ni pamoja na:

1.   Kuchunga mambo ya umma, maslahi yao pamoja na kutatua matatizo yao na kukidhi haja zao.

2.   Kutetea haki za umma katika nyanja zote za dini, uchumi, siasa, fikra, tabia na jamii kwa ujumla.

3.   Kuhifadhi umoja wa umma na kuuunganisha ikiwa ni pamoja na kulinda heshima na utukufu wake.

4.   Kuuongoza kueleka ukamilifu na kuuelekeza kunako yeye kuleta furaha ya dunia na akhera.

5.   Kuutoa katika dhulma na ufisadi na kukengeuka, ikiwa ni kwa kuweka misingi ya kuamrisha mema na kukataza maovu.

6.   Kusimamisha mambo ambayo kwayo jamii itasimama sawia.

7.   Kusimamia majukumu ya kijamii ambayo hayafai kuachwa,kama vile kusimamisha sala ya Ijumaa, kupangilia mambo ya jeshi, kupangilia matumizi ya mali za umma, kuzingatia uadilifu kwa wastahiki wa mali na vitega uchumi kama vile ardhi na umma na mengineyo.

8.   Kuchunguza mizozo na shubuha maalumu, ambazo si katika kazi za mufti tu bali hata kiongozi na mtawala wa umma anafaa kusimamia. Kama vile kubainisha mwanzo wa miezi, uchafuzi wa sehemu tukufu ambao uaweza kupelekea nguvu za silaha kutumika hapo nk.

Na hizi ni baadhi tu ya anuani ambazo chini yake kunaweza kupatikana mengine mengi yanayoweza kuchambuliwa katika sehemu maalumu.

Kwa ufupi i kwamba Faqih ambaye ametimiza vigezo vyote baada ya kuwa ndio naibu wa Imamu Mahdi as, (kwa anuani ya unaibu wa ujumla na si mahususi), anakuwa na majukumu yote ambayo Mwenyezi Mungu ameyaweka kwa Imamu (as), katika yote yanayohusiana na kupangilia mambo ya umma kidini na hata kidunia, hasa katika mambo ambayo Imamu wetu aliye mafichoni inakuwa ngumu kwake kuyapangilia kutokana na kupingana kwake na mipango ya Mungu katika kumficha kwake. Isipokuwa tu Imamu atabakia na sifa zake nyingine kama vile Kutofanya makosa (Ismah) na kuja na habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu swt.

Na dalili katika kuonyesha unaibu wa Kiongozi ni dalili ile ile yenye kuthibitisha ulazima wa kuwepo Imamu, ambapo ni akili inahukumu kwamba ni lazima Imamu awepo ili kuweza kulinda miji na kupangilia maisha ya waja kidunia na akhera pia.

Imamu Ally as katika kuelezea ulazima huu anasema:

“...Li lazima watu wawe na kiongozi, kiongozi ambaye katika uongozi wake muumini atatenda mambo yake, na kafiri atasikiliza amri zake, ambaye kwaye muda na wakati wa Mungu utafika, watu watakutanishwa, adui atapambana, njia zitakuwa salama, dhaifu atachukua kutoka kwa mwenye nguvu, mpaka pale mwema atakapopumzika au kupumzishwa na muovu...”[1]

Sasa kwa minajili ya ulazima huu, pia tunatambua kwamba ni lazima huyu Faqih awe ni kwa misingi ya Mungu. Kwa maana ni lazima awe mjuzi wa kanuni za kimungu na awe na uwezo wa kudurusu na kutoa dalili za kisheria kutoka katika chimbuko lake.

Pia awe na kiwano cha juu cha kuepukana na matamanio ya nafsi na kuelekea dunia, bali awe ni mtu wa Mungu kwa kiasi kwamba uwepo wake wote uwe ni kumueleka Mungu tu.[2]

Na katika hili kuna masiala kadhaa:

1.   Mwanamke hana vigezo vya kutawala mambo ya umma.

2.   Kama ambavyo Imamu mwenye kutimiza vigezo ni naibu wa Imamu, vile vile ni naibu wake katika kuchukua majukumu na kutekeleza yale ambayo Imamu alikuwa akitekeleza. Tumetaja baadhi yake katika kitabu cha “..Daurul Aimmah Fil Hayatil Islamiya”.

3.   Pindi ambapo nidhamu na mfumo wa kisiasa hautakuwa kwa mpango ni nidhamu ya Kiislamu, na ikawa huyu kiongozi wa Umma hana mamlaka makubwa, basi inatosha kwake kutoa idhini kwa dola ya wakati huo kutekeleza baadhi ya majukumu kama vile kuhifadhi nidhamu na mifumo ya kijamii, na kwa minajili hiyo dola inakuwa ni kama vile wakili wake katika utekelezaji. Na kwa minajili hii kila jambo ambalo dola italisimamia kama vile kujenga taasisi mbalimbali, mmiliki wake wa asili anakuwa ni Imamu (as), na hata katika kuzitumia pia itahitajika idhini ya naibu wa Imamu ambaye ni Marji sasa. Na wala hazitakuwa mali hizi ni katika zile mali ambazo mmiliki wake hajulikani au katika mali zenye kumilikiwa kwa kuhodhi na kuwahi.

4.   Faqih hana haki ya kueneza utawala wake kwa watu kwa kutumia nguvu na mabavu, bali ni sharti kuwaridhisha juu ya utawala wake huo.

Sawa tunaposema Umma hatumaanishi umma wote, kwa maana hata kumchagua kiongozi huyu hakusimamii uchaguzi ambao utafanyika na watu wote. Hivyo tunaposema Umma tunamaanisha wale wenye upeo katika nyanja hii ambao ni walimu wa vyuo vya dini wenye kusifika na Uchamungu, kuepuka mabaya, maarifa juu ya mambo ambayo jamii inayahitajia katika kusimika sheria za Kiislamu.

 

5.   Ni wajibu wa Faqih kuwa imara  katika nyanja ya maneno na matendo yake kwa kadri ambavyo Mwenyezi Mungu anamfanyia wepesi, ili tu kuweza kuwakinaisha watu kunako Uislamu na nidhamu yake, kama ambavyo pia ni lazima awe na uwezo wa kuongoza watu kuelekea ukamilifu na usalama.

1436 Hijiria

Mwaka 2015 Miladia.



[1] Nahjul Balagha hituba ya 40 kuwazungumzia khawarij baada ya kuinua kauli mbiu ya kwamba Hakuna hukumu ila ni ya Mwenyezi Mung utu.

[2] Ilalu Sharai cha Sheikh Saduq