Mwanzo | | Maneno ya maadili | Kutumwa Mtume (s.a.w.w)
Kutumwa Mtume (s.a.w.w)

Shiriki swali

Kutumwa Mtume (s.a.w.w) ni miongoni mwa neema kubwa za Mwenyezi Mungu

Katika neema kubwa za Mwenyezi Mungu ni Mtume Muhammad (s.a.w.w) kupewa utume, tukio ambalo leo hii tunaishi kumbukumbu zake. Kutumwa kwake (s.a.w.w) kulileta mapinduzi makubwa mno katika hostoria ya mwanadamu, kiasi kwamba jamii iliyokuwa nyuma, wakiuwana wao kwa wao na kujifakharisha kwa kutend machafu na jinai kama vile: kuwazika watoto wakike wakiwa hai, uznzi na unywaji pombe. Ilikuwa ni jamii iliyosambaratika na isiyokuwa na mshikamano, huku ikiwa imezungukwa na madola yenye nguvu yakisubiri kuivamia, ni jamii iliyokuwa imekusanya kila aina ya maovu na ufisadi. Lakini kwa baraka ya Mtume (s.a.w.w) ikaja kuwa ni jamii iliyoendelea na yenye nidhamu madhubuni, ikiuongoza ulimwengu, ikiuongoa ubinadamu, na kuwapatia walimwengu kanuni bora iliyobeba dhamana ya utukufu, furaha na kheri yao.

total: 1 | displaying: 1 - 1

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf