Tamko la Mwisho la Ziara ya Arobaini kwa mwaka 1443Hijiria

| |defa okundu : 663
Tamko la Mwisho la Ziara ya Arobaini kwa mwaka 1443Hijiria
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Çıktı al
  • save

Kwa jina la Allah

 

Tamko la Mwisho la Ziara ya Arobaini kwa mwaka 1443Hijiria

 

[Alhamdulillah! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye aliye tuongoza kufikia haya. Wala hatukuwa wenye kuongoka wenyewe ingeli kuwa Mwenyezi Mungu hakutuongoza. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walileta Haki].

Amani iwe juu ya Husein na iwe juu ya Ali bin Husein, na amani iwe juu ya Abul-Fadhil-Al Abbasi, na amani iwe juu ya watoto wa Husseini, na amani iwe juu ya maswahaba wa Husseini ambao walitoa uhai wao kwa ajili ya Husein (a.s)

, na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake ziwe juu yao.

 

       Mwaka huu na kama ilivyo kila mwaka, mamilioni ya waislamu wapenzi wa njia ya Imamu Husein (a.s) ,wametowa ujumbe wa uadilifu, furaha, amani, upendo na udugu kwa wanadamu wote. Vilevile wametoa ujumbe wa kupinga dhulma, utumwa, ubeberu na unyonyaji, kupitia kwenye matembezi na masira ya mamilioni ya watu yanayo fikia umbali wa mamia ya kilometa, matembezi ambayo yanadhihirisha misingi ya kibinadam iliyo tukuka.

 

       Nchini Iraq tunapotoa huduma zote hizi bure kwa mazuwari wa Imamu Husein (a.s) zaidi ya milioni kumi kwa muda wa masiku kadhaa, hatufanyi hivyo kwa lengo la kumsimanga yeyote, wala hatutarajii kutoka kwa yeyote malipo wala shukrani, isipokuwa tunalichukulia hilo kuwa ni wajibu wetu na ni sehemu ya kutoa shukrani zetu kwa Mwenyezi Mungu ambaye ndiye mnemeshaji, kwa kuichagua ardhi yetu tukufu iwe ndio makazi ya mawalii wake watakatifu na kutuchagua sisi tuwe ndio wakazi wa ardhi hii. Hivyo, ni wajibu wetu kuwakirimu mazuwari wa mawalii hao, kwa namna ambayo itatufanya tuwe wastahiki wa neema hii, na ili kuandaa dola la uwadilifu wa Mwenyezi Mungu ambalo litasimamishwa na Imamu Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe ujio wake)  kwenye ardhi hii iliyobarikiwa na kuifanya makao makuu yake, ambapo kutokea hapo ataujaza ulimwengu amani, salama na neema.

 

       Hakika wapinzani hutotolea dosari na kasoro kwasababu ya matembezi haya, na wamezua shubuhati na mashaka mengi dhidi yetu!  Lakini hayo ni kwasababu hawana baswira na muono wa mbali wa kuweza kuona utukufu na baraka za matembezi haya matukufu kwa wanadamu wote, aliotangulia, waliopo na mpaka kwa wale wajao. Na inatosha kufahamu utukufu wa matembezi haya kuwa ni kudhihirisha upendo kwa watu wa nyumba ya bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambao Mwenyezi Mungu ameamuru kuwapenda aliposema katika kitabu chake kitakatifu:

 

[Sema: kwa haya siombeni malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu (Ahlubayti)].

 

Lakini pia jambo hilo limekuwa ni sababu ya watu wengi kuongoka kwenye njia ya haki, na kutoa kiapo cha utii kuendelea kupita kwenye njia ileile waliyoipata mashahidi, wakweli na watu wema.

 

       Wapinzani wanautaka tuwatolee muujiza unaothibitisha ukweli wa marasimu hii, lakini ni wingi ulioje wa miujiza kwa wenye akili na uelewa! Moja kati ya miujiza hiyo ni haya maadili mema na hali ya juu yanayodhihirishwa na washiriki wa marasimu hayo, kiasi huwa na kutoa, ikhlasi na kujitolea kwa hali ya juu kabisa, namna ambayo mfano wake haipatikani katika ulimwengu wa leo ulioghiriki katika katika mambo ya kidunia.

Na sasa tunawaonesha moja miujiza hiyo, ambao ni kwamba, masira na matembezi yanakusanya wazuwari zaidi ya milioni kumi wanatembea wakiwa wamekaribiana kwa muda wa masiku kadhaa, na wakikusanyika katika maeneo mafivyu. Lakini hata hivyo, vituo vyote vya tiba tulivyouliza na vilivyokuwa kwenye njia ya mazuwari hao, hawakusajili wala kuripoti tukio lolote lile la maambukizi ya Korona lilithibitishwa.

        Na kwamba uchunguzi wa kila siku wa maambukizi ya Korona unaofanywa katika mikoa yote ya Iraq, ambapo kabla munasaba wa Arubaini yalikuwa yanazidi elfu kumi, unaonyesha kuwa katika masikio Arobaini, idadi ya maambukizi ilipungua hadi kufikia elfu mbili! Wakati ambao maelfu ya watu waliohudhuria katika uwanja wa Landon mwezi wa sita mwaka huu walisababisha kuongezeka maambukizi kwa namna ambayo haina mfano. Kiasi kwamba idadi ya maambukizi ilipita elfu hamsini kwa siku moja! Hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa nusu ya wakazi wote wa Ujerumani walikuwa wamekwisha chanjwa chanjo dhidi ya Corona! Na jambo la kushangaza, hii ilitokea siku ambayo iliamuliwa kuondoa vizuizi kwa sababu ya Corona, na waliiita Siku ya Uhuru.

       Angalizo: Ni kwamba maneno yangu haya hayana maana ya kuwataka watu wakeuke taratibu za kujilinda zilizowekwa na wahusika, isipokuwa ninazungumzia jambo la kweli lililotokea.

 

       Kwa hakika alama za Mwenyezi Mungu zina nafasi kubwa katika kusimamisha dini na kuimarisha imani na itikadi katika nyoyo za watu, na siwezi hata kufikiria hali za watu zitakuwaje iwapo wataishi bila kufuta alama hizo la Mwenyezi Mungu. Bila shaka watarudi katika ujahilia wao wa mwanzo kama ilivyotokea katika nyumati zilizopita, pindi zilipojitenga na mafunzo ya manabii qaongofu.

 

       Tunamuomba Mwenyezi Mungu azidumishe neema zake juu yetu, aihifadhi Iraq yetu pendwa, na ayalinde mataifa yote ya kiislamu kutokana na vitimbi vya maadui, ubaya wao na  uovu wao. Na atuimarishe katika njia ya msimamo, kwa hakika yeye ndiye walii wa kila neema.

Muhammad Yaqoobi-Najaf Ashraf

20/Swafar/1443 Hijiria

28/09/2021