Marjii Yaqooobi katika kikao chake na msafara wa wito wa Al-aqsaa alisema: “Hakuna mbadala wa chaguo la Uislamu katika nyanja zote za mapambano na maadui”.
Kwa jina la Allah
Marjii Yaqooobi katika kikao chake na msafara wa wito wa Al-aqsaa alisema: “Hakuna mbadala wa chaguo la Uislamu katika nyanja zote za mapambano na maadui”.
Samahat Marjii wakidini, sheikh Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) amekutana ofisini kwake katika mji wa Najaf Ashraf 1, na msafara wa (Nidaul Aqsaa) ulikuwa umekusanya kundi la wanazuoni wa dini ambao ni wanamapambano masuni na mashia kutokea Palestina, Siria na Lebanoni, ambao walikusudia kuweka maukibu na kituo chao katika njia mazuwaru wa Imam Husseini (a.s) kwa lengo la kuwahimiza waumini juu ya kuendelea kuikumbuka Qudsi na kubakisha taa la Jihadi na mapambano likiwa ni lenye kuwaka mpaka zitakaporejeshwa ardhi za Palestina zilizoporwa na wazayuni.
Baada ya wanamsafara kueleza malengo yao ya uamuzi waliochukua na kufafanua taabu na matatizo ya raia wa Palestina na uimara wao katika kukabiliana na taabu hizo, ndipo Samahat Marjii (Allah amhifadhi) alipoanza mazungumzo yake kwa kuukaribisha msafara, akiashiria juu ya neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa ameukusanya ugeni huo katika eneo lenye mahususi na lenye sifa za pekee, eneo ambalo ni kuwa jirani na karibu kabisa na Imam Ali bin Abi Twalib (a s), ambaye ni mng’oa mizizi ya vitimbi na fitina za Mayahudi katika vita endelevu za Uislamu. Na neema nyingine aliyoiashiria ni ile ya Mwenyezi Mungu kuwakutanisha katika wakati maalum na wenye hususia maalum, kwani sasa tunaishi kumbukumbu za mapinduzi ya Imam Husseini (a.s) ambaye ni nembo ya Jihadi na mapambano na kupinga dhulma, lakini pia ni kigezo chema kwa wapambanaji na wapigania haki na kwa wote wenyekutetea uhuru wa mwanadamu. Kisha akaendelea kusema:
Kwa hakika Msikiti wa Aqsaa ni kibla cha kwanza na ni haramu ya tatu baada ya ile ya Makkah na Madina. Na sehemu hiyo ina nafasi na heshima maalum katika nyoyo za waislamu tangu mwanzoni wa Uislamu. Na marajii wa kidini katika mji wa Najaf Ashraf, alilipa suala la Palestina Qudsi umuhimu mkubwa tangu zama za hapo mwanzo kabisa. Kwa hakika Marjii wa kidini na mwanaharakati mkubwa, Marehemu Sheikh Muhammad Hussein Aali Kashiful Ghitaa (Allah audumishe utajo wake), alishiriki mwenyewe katika kongamano la kiislamu ambalo lilifanyika katika Qudsi (Palestina) mnamo mwaka mwa 1350 Hijiria sawa na 1931 Miladia, mwanzoni harakati ya Mayahudi kuhamia katika ardhi ya Palestina baada ya ahadi ya Balfur mwaka 1917 Miladia.
Samahat Marjii, ameendelea kuonyesha ushirikiano wa marajii wa Najaf Ashraf (2) na uungaji wao katika harakati za kijihadi na kimapambano dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni mwaka 1969, pindi kulipofanyika kitendo cha kutoa muhanga, baada ya tukio la kuchomwa moto muskiti wa Aqsaa, kiasi kwamba Marjii wa kidini wa juu kabisa katika mji wa Najaf Ashraf kwa wakati ule, Samahat Sayyid Muhsin Al-Hakeem (Allah audumishe utajo wake), alibariki na kuunga mkono hatua na akatoa idhini ya kutumiwa mali za kisheria zitolewazo na wafuasi kwa Marjii katika matendo kama hayo. Na kwamba, marjii wa kidini wakati wote wamekuwa wakiwataka wapambanaji na wanaharakati kufuata chaguo la Uislamu katika mapambano yao dhidi adui wao, kwani adui haingii vitani nao isipokuwa ni kwa msingi imani anayoibeba na hivyo hupambana kwa ajili ya imani hiyo, ndio maana hapana budi kupambana na kukabiliana naye kwa imani na itikadi pia.
Lakini, kwa bahati mbaya, serikali tawala ikiwa ni katika kutekeleza ajenda za wadhamini wao wanaowasukuma kufanya kila kitu, zilipaza nara za utaifa na uarabu ambazo hazikutosha kuwa na msukumo wa kujitoa muhanga kwasababu ya kutoambatana na itikadi na imani ya Uislamu.Na hivyo wakawa wameweza kuyatenga mbali mataifa yote ya kiislamu na mapambano kwakueneza uvumi kuwa suala la Palestina haliwahusu na kwamba ni jambo la waarabu tu.
Kwa upande mwingine, Samahat Marjii ameeleza kuwa, hata hivyo mnamo mwaka 1978 Miladia mambo yalibadilika, pale wanamapambano walipoamua kuchukua chaguo la Uislamu na kuachana na utaifa na uarabu, na huo ukawa ndio mwanzo wa kusonga mbele harakati ya mapambano ya kiislamu na nguvu ikaongezeka pamoja na nguvu zake, ambayo ndio ile nguvu aliyoiashiria Mwenyezi Mungu Mtukufu pale aliposema:
[Wakiwapo kati yenu ishirini wanao subiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo kati yenu mia watawashinda elfu moja katika walio kufuru].
Kisha Mwenyezi Mungu anatoa sababu ya makafiri kushindwa mwishoni mwa aya hiyo kwa kusema:
[Kwa sababu wao ni watu wasio fahamu].
Hali kadhalika, Samahat Marjii ameashiria juu ya mabadiliko ya linguino wa nguvu kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa maslahi ya wapambanaji. Kwani baada ya kuwa walikuwa wakipambana na maadui wao wazayuni kwa kuwatupia mawe wakati wao wakipigwa risasi hali yakuwa vifua vyao viko wazi bila ya ngao, lakini katika mapambano ya hizi karibuni ya -Seiful Qudsi- wamefurumusha maelfu ya makombora vichwani mwa maadui na yanaweza kuingia kwenye miji ya utawala haramu wa kizayuni.
Na hatimaye, mwishoni mwa kikao hicho, wageni wa msafara walionyesha furaha yao ya kukutana na Samahat Marjii ambaye amekata kui yao kwa pale aliposema kuwa marajii wa mji wa Najaf Ashraf alikuwa na wataendelea kuwa ni nguzo na tegemeo juu ya suala la Palestina na kwamba wataendelea kuliunga mkono na kulisimamia.
ـــــــــــــــــ
[1] – Tarehe ya kukutana ni Jumatatu 12 mwezi Swafar 1443Hijiria, sawa na 20/09/2021 Miladia.
[2] – Samahat Marjii Yaqooobi (Mwenyezi Mungu amhifadhi) ametoa msimamo hadhaa kuhusiana na suala la Palestina, miongoni mwa misimamo hiyo ni pamoja na:
a) Kitabu (Nadhrat Fii Falsafatil Ahdaath) ambacho barua alizotumiana na mwalimu wake Shaheed Sadr (Allah audumishe utajo wake), katikati kwa miaka ya themanini karne iliyopita.
b) Waraka wa kumuombeleza Sheikh Ahmad Yaasin.
C) Hotuba aliyoitoa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Qudsi.
Na yote hayo yalikusanywa katika kitabu kidogo kilichoitwa: Palestina na Qudsi katika dhana ya Najaf Ashraf(Falestinu wal-Qudsu Fii Dhwamiirin Najafil Ashrafi).